Kama wewe ni mtumiaji mzuri wa mtandao wa Twitter Blue utagundua kuwa kuna mabadiliko yamefanyika na kwa kiasi kikubwa yanahusisha picha na maneno.
Twitter Blue mara kwa mara imekua ikijitahidi katika kuboresha vipengele au hata kuleta vile vipya zaidi ambavyo kwa namna moja au nyingine vitawafaa watumiaji wa mtandao huo.
Kumbuka zamani watumiaji wa twitter walikua na uwezo mpaka wa kuandika maneno yanye herufi 10,000 wakati kwa sasa kuna ongezeko mpaka la herufi 25,000.
Zamani ilikua ni lazima katika tweet maneno yaanze na kisha kwa chini ndio kunakua na picha husika lakini kwa sasa hili linabadilika.
Sasa utakua na uwezo hata wa kupost maneno kidogo kisha ukaweka picha na kisha kwa chini kabisa ukamalizia na maneno mengine.
Hii itakua haina tofauti kubwa sana na machapisho katika mitandao mbalimbali kama vile mtandao wetu pendwa wa TeknoKona.
Kingine ni kwamba ukifikiria sana juu ya hili utagundua kwamba hapa kampuni kwa kina imewalenga waandishi mbalimbali na hata watu wa blogu (bloggers)
Kwa sasa huduma hii inapatikana kwa watumiaji wa Twitter Blue tuu, pengine inaweza kuja katika mtandao wa Twitter wa kawaida hivyo hatuna budi kusubiri
Ningependa kusikia kutika kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani ni hatua sahahi imechukuliwa na Twitter au mambo yangebaki vile vile tu.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.