Kampuni nguli ya utengenezaji wa simu duniani, Samsung imetangaza kwa watumiaji wa simu za matoleo ya Galaxy Note 9 na Galaxy S9 kwamba watapata masasisho ya Android 9 Pie kuanzia mwezi Januari mwaka 2019.
Taarifa hiyo imetolewa rasmi kwenye mkutano wa mwaka wa wakuzaji wa bidhaa za Samsung 2018 (SDC 2018) uliofanyika huko San Francisco, Marekani.
