fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
apps Teknolojia

Kiswahili kutumika katika Microsoft Translator

Kiswahili kutumika katika Microsoft Translator

Spread the love

Kampuni ya Microsoft imezindua tafsiri ya maandishi ya lugha ya Kiswahili, lugha ya kwanza ya Kiafrika kuweza kutafsiriwa katika programu ya kutafsiri lugha iitwayo Microsoft Translator, inayomilikiwa na kampuni hiyo.

Mfumo huo wa tafsiri uliundwa kwa kushirikiana na watafsiri wasio na mipaka (Translators without Borders), asasi isiyokuwa ya kiserikali yenye lengo la kuongeza upatikanaji wa elimu na ufahamu kupitia tafsiri za maana.microsoft translator teknokona

Lugha ya Kiswahili inazungumzwa na watu wapatao milioni 150 katika ukanda wa Afrika Mashariki zikiwemo nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Msumbiji na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Tafsiri kwenda lugha ya Kiswahili itakuwa inapatikana kupitia programu ya Microsoft Translator kwenye vifaa vinavyoshabiiana na programu hiyo, hivyo kuwawezesha watu binafsi na mashirika kupata tafsiri ya haraka kwa gharama nafuu. Mfumo huo wa tafsiri unalenga katika kuongeza upatikanaji wa elimu pamoja na kuhimiza mawasiliano kati ya watu wenye tamaduni tofauti kwa kujenga mifumo mipya ya lugha.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo,  Meneja Mkazi wa Microsoft nchini Kenya, Kunle Awosika alisema kuwa kupitia mfumo huo mpya wa tafsiri, serikali katika ukanda wa Afrika Mashariki zitakuwa na uwezo wa kuandaa nyaraka na taarifa zilizopo katika lugha za kigeni kupatikana katika lugha ya Kiswahili pasipo gharama yoyote. Aidha, serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali watakuwa na uwezo wa kuwasiliana na wananchi kwa haraka, na muhimu zaidi, watu watakuwa na uwezo wa kuwasiliana na watu walio nje ya mipaka yao kwa madhumuni ya kibiashara au binafsi.

“Kuongeza lugha ya Kiswahili kunatuleta hatua moja karibu na lengo kuu ambalo ni kuondoa vikwazo vya lugha kwa kuruhusu watu kutafsiri kitu chochote, mahali popote na wakati wowote. Wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili Afrika Mashariki na duniani kote sasa wanaweza kupata taarifa nyingi za habari na utamaduni, na wanaweza kuingiliana na wazungumzaji wa lugha 50 zilizopo katika programu ya Microsoft Translator. Kikubwa zaidi, wazungumzaji wa lugha hizi duniani kote sasa wanaweza kupata moja kwa moja historia na utamaduni wa wakiswahili kwa upana zaidi,” alieleza Bw Awosika.

SOMA PIA  OnePlus kuanzisha biashara nyingine

Microsoft Translator imejumuishwa katika bidhaa mbalimbali za Microsoft ikiwa ni pamoja na Bing, Microsoft Office, (Word, Word Online, PowerPoint, Excel, Outlook, Publisher, OneNote, na Visio), SharePoint, Cortana, na Yammer. Pia ina kifurushi kamili cha programu kwa ajili ya Kompyuta na simu za mkononi ikiwa ni pamoja na  Windows, Windows Phone, Android and Android Wear na iPhone and Apple Watch ambacho kitawezesha mawasiliano katika nyakati ambazo tafsiri ya haraka, uhakika na gharama nafuu itahitajika.

SOMA PIA  Tuzo ya mwaka kwa Tecno Phantom 8

Microsoft Translator Web Widget itawezesha watu binafsi na mashirika kuongeza kwa urahisi msaada wa kutafsiri lugha mbalimbali katika tovuti zao bila gharama yoyote. Kiswahili pia kitapatikana kama lugha ya kutuma ujumbe katika programu ya kompyuta ya Skype. Aidha, watengenezaji wa programu wataweza kuunganisha tafsiri ya Kiswahili katika bidhaa na programu zao kupitia Microsoft Translator API.

Kwa taarifa zaidi juu ya Microsoft Translator, tembelea:

(Chanzo – Microsoft, Dar es Salaam)

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Comments

  1. […] post Kiswahili kutumika katika Microsoft Translator appeared first on […]

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania