Mtandao maarufu wa YouYube umekuja na huduma spesheli wanayoiita YouTube Red ambayo itakulazimu ulipie takribani dola 10 kwa mwezi. Kwa wengi hii inaonekana mtandao huo unaenda katika kushindana na mitandao mingine kama vile Netflix inayotoa huduma spesheli za video ambazo huitaji watumiaji kulipia kila mwezi.
Kwa takribani elfu 20 kwa mwezi utaweza kuangalia video bila matangazo, pia kuweza kuchagua baadhi ya video kuweza kuziangalia ata kama hauna huduma ya intaneti/data, pia kwenye simu yako utaweza kuendelea kusikiliza video yako kwenye simu yako. Kwa sasa huduma hiyo itaanza kupatikana nchini Marekani ila baadaye huduma hiyo itaanza kupatikana katika nchi zingine nyingi zaidi.
Huduma ya YouTube Red isiyokuwa na matangazo itaanza kupatikana wiki ijayo huku kuanzia mwezi wa kwanza watumiaji wa huduma hiyo wataanza kupata tamthilia, filamu na mengineyo. Wakati uwezo mwingine utaanza kuongezwa taratibu.
Pia kuzidi kuifanya huduma hiyo kuwa tamu zaidi watu wanaolipia huduma ya YouTube Red watapata pia huduma ya Google Play Music bure kabisa. Huduma ya Google Music inafanana na ya Spotify ambayo ni huduma inayokupatia huduma ya kusikiliza nyimbo mbalimbali bila haja ya kuzishusha (download) kwenye simu au kompyuta yako.
Je unadhani kibongo bongo unaweza kulipia huduma kama hii kwa zaidi ya Tsh 20,000 kwa mwezi? Kisa matangazo tuu, tuambie maoni yako.
2 Comments