WhatsApp ni Application ya simu inayokuwezesha kutuma meseji na media kwa ujumla. Zaidi ya Watu milioni 500 wenye Simu-janja duniani wanatumia whatsApp kwenye simu zao. Sababu ya umaarufu wa whatsApp ni wa kawaida sana na ni kwasababu ni moja kati ya App nzuri za kutuma na kupokea meseji na ina vipengele (features) vingi hivi sasa. Lakini tatizo la WhatsApp ni kwamba Haisapoti simu zote, inapatikanaa kwa baadhi ya simu tuu. Vipi wale wasio na simu zinazowawezesha kupata whatsApp? vipi kama umeibiwa simu yako amabayo ilikua na WhatsApp?. Zifuatazo ni Njia Za Kijanja zitakazo kuwezesha kuipata WhatsApp kwenye Kompyuta Yako.
A: Wezesha Kwa Kutumia Bluestacks
Hi ndio njia Rahisi na maarufu sana kwa wale wanaotumia whatsApp kwenye kompyuta zao. Njia hii haina mbwembwe nyingi, kila mtu anaweza tumia kwa kufuata maelekezo kidogo
1. Kwanza kabisha shusha Bluestacks toleo la 0.8.1.3011 hapa
2. Ikishamaliza Anza Instillation
3. Ukishamaliza Instillation kibox hiki kitatokea
4. Baada ya Hapo Bonyeza AppStore Kisha Tafuta na Shusha WhatsApp
5. Ikiwa Tayari ifungue kisha Hakikisha namba yako kwa kuanza kutumia.
B. Wezesha Kwa Kutumia YouWave
Unaweza Pia Pata whatsApp kwenye Sotware ya Youwave. Youwave inakuwezesha kupata Apllication zote za Adroid katika kompyuta yako. Kitu kizuri kuhusu hii ni kwamba unaweza cheza magemu ya Multiplayer na pia inawezekana kuingia kwa kompyuta zinazoingiza Os za windows xp, windows 7, windows 8 na windows vista.
Unaweza Shusha YouWave Hapa. Ukishamaliza instillation unaweza wezesha Applikeshini za Android kama WhatsApp.
Kuna Njia Nyingi sana za kukuwezesha kutumia whatsApp kwenye Kompyuta yako na nyingi zinafanana fanana kwa kuwa zinakua katika mfumo wa android. Kwa kutumia njia hzo sasa wale wasio na simu zinazoruhusu WhatsApp Watakua wanakula sahani moja na wale wenye ma Simu-janja zao.
Ningependa sikia kutoka kwako, Niambie kwenye comment Njia Hizi Umezipokeaje?
No Comment! Be the first one.