fbpx
Kompyuta, Microsoft, Teknolojia, Windows, Windows 10

Unatumia Windows 7? Muda wa kwenda Windows 10 umefika.

unatumia-windows-7-muda-wa-kwenda-windows-10-umefika
Sambaza

Kama unatumia Windows 7 kwenye kompyuta yako basi muda wa kusasisha (upgrade) kwenda Windows 10 umefika. Microsoft wameiweka tarehe 14 Januari 2020 kama mwisho rasmi wa utumiaji wa Windows 7.

windows 10 updates masasisho kompyuta Unatumia Windows 7

Je ni nini kitatokea?

Kuanzia tarehe 14 January kompyuta inayotumia Windows 7 isitegemee kupata updates (masasisho) ya aina yeyote ya kuhakikisha usalama wa data kwenye kompyuta zao.

Microsoft, wanalenga watumiaji wote wahamie katika programu endeshaji yao ya kisasa ya Windows 10.

INAYOHUSIANA  iPhone 12 Pro Max na picha zake za awali

Kutumia toleo la Windows ambalo halipati masasisho (updates) ya kiusalama ni hatari kwa usalama wa data zako. Kompyuta zinazotumia Windows 10 zinakuwa katika hatari kubwa ya kushambuliwa na virusi au programu za udukuzi wa data (ransomware).

utumiaji wa windows 7
Utumiaji wa Windows 7 unaendelea kupolomoka, kama bado unatumia Windows 7 ni muda wa kuachana nayo

Soma zaidi kuhusu Windows 10;

Data kutoka shirika la data la NetMarketShare linaonesha utumiaji wa Windows 10 kukua, kufikia Disemba mwaka 2019 asilimia 54.62 ya kompyuta zinazotumia intaneti zilikuwa zinatumia Windows 10, huku Windos 7 ikichukua asilimia 26.64 tuu. Asilimia zingine zikichukuliwa na Mac OS, Linux na matoleo mengine ya programu endeshaji.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |