Caption: Programu ya utafutaji wa Subtitles kwa njia rahisi (Windows/Mac)

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Caption, ni programu inayorahisisha utafutaji wa subtitles. Kuna tovuti nyingi kwa ajili ya kupata subtitles, ila programu ya Caption inafanya utafutaji huo kuwa ulio rahisi.

Programu ya Caption ni nyepesi, ila inahitaji huduma ya intaneti katika ufanyaji kazi wake. Itahitaji udondoshe (drag) file la muvi au tamthilia unayohitaji subtitle yake.

Kwa kufanya hivyo programu hiyo itakutafutia subtitle na ikiipata itaidownload moja kwa moja kwenye folda la muvi yako.

INAYOHUSIANA  Jinsi ya Kulogout Skype sehemu uliyoisahau! #Maujanja

Pia una uwezo wa kuandika jina la muvi au filamu na programu hiyo itakutafutia, na kukuletea orodha ya subtitle unazoweza kudownload.

caption programu ya utafutaji subtitle

Caption, ni programu ya utafutaji subtitle inayopatikana bila malipo

Programu hii ni ya bure na unaweza kuipata kwa kutembelea tovuti hii – > Caption

Je wewe huwa unatumia njia gani kupata subtitles pale unapozihitaji?

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.