fbpx

Windows 10 Itaingia Ktk Kompyuta Zenye Uwezo Huu!

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Mara nyingi tumekutana na hili jambo ambapo watu wanaotuzunguka wanauliza kama kompyuta zao zina uwezo wa kupokea programu endeshaji ya windows 10.

Hii inaweza ikawa mtu anataka kusasisha toleo la mbele zaidi baada ya kuwa anatumia toleo la nyuma (windows XP, windows 7 n.k). Sasa ili kupata toleo kubwa kabisa inabidi kompyuta yako iwe na sifa fulani

Logo YA Windows !0 Na Windows 7

Logo YA Windows !0 Na Windows 7

Cha msingi kujua hapa ni kwamba kama kompyuta yako tayari ina windows 7, kuna hati hati kubwa kuwa itaruhusu toleo la windows 10 bila tatizo lolote. Kwa kifupi ni kwamba windows 10 na windows 7 zina mahitaji sawa ila kukaa katika kompyuta husika.

INAYOHUSIANA  Smart TV: Jinsi ya kuzuia isidukuliwe

Mahitaji  Hayo Ni Haya Hapa!

  • CPU: 1GHz au zaidi
  • RAM: 1GB kwa ajili ya 32-bit Windows au 2GB kwa ajili ya 64-bit Windows (au zaidi)
  • Hard Disk: 32GB au zaidi
  • Graphics Card: Inayoendana na DirectX 9 au mpya zaidi yenye driver ya WDDM 1.0 

Ni wazi kuwa window 10 na 7 zinashabihiana katika swala zima la mahitaji ina kuna utofauti mdogo sana baina ya wawili hao. Windows 10 kwa haraka haraka ni lazima itakuwa inahitaji ujazo mkubwa wa hard disk ukilinganisha na windows 7.

Laptop Yenye OS Ya Windows 10

Laptop Yenye OS Ya Windows 10

Mpaka hapo nadhani utakua huna maswali mengi juu ya ni windows ya aina gani inaweza ikaingia katika kompyuta yako kwani TeknoKona imekufumbua macho leo.

INAYOHUSIANA  Waathiriwa wa Samsung Galaxy Note 7 wabadilishiwa simu

Chanzo: Microsoft

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini sehemu ya maoni, Tembelea mtandao wako pendwa kila siku. Kumbuka TeknoKona daima tupo nawe katika teknolojia!

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.