fbpx

Xiaomi yaendelea kukua kwa kasi

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Kampuni ya simu, Xiaomi imebainisha kuwa kwa sasa biashara yake imepanuka zaidi katika sehemu tofauti duniani mbali na Uchina.

Hayo yalibainishwa na mfanyabiashara, bilionea na mmiliki wa kampuni hiyo ya Xiaomi, Bw. Lei Jun wakati wa jukwaa la biashara na uwekezaji lililofanyika Shanghai ambapo masoko ya Xiaomi nje ya Uchina yamefikia takribani 82 na matano kati yao yakiwa ya kiwango cha juu kati ya masoko 25 makubwa duniani.

Xiaomi yaendelea kukua

Biashara ya soko la nje ya Uchina limewapa faida kubwa kwa kuwabadilisha watumiaji wengi na kuanza kutumia bidhaa zao.

Soko la simu za Xiaomi zimeendelea kukua hususani robo ya pili ya mwaka 2018 kwa kukua kwa asilimia 150 ingawa wengi wakisema kampuni hiyo bado ni ndogo.

Xiaomi yaendelea kukua

Baadhi ya bidhaa za Xiaomi: Kwa mujibu wa Lei Jun lengo la Xiaomi ni kuleta bidhaa zenye ubora kwa watumiaji wa aina zote.

Xiaomi iliyoanzishwa mwaka 2010 na kuanza kusambaa duniani kuanzia mwaka 2014, asilimia 95 ya simu zake kwa soko la Indonesia na India zinazalishwa ndani ya nchi hizo.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Samsung Galaxy Note 10 kuja katika matoleo manne tofauti
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.