Samsung Hizi Ndio Zinazokubali Teknolojia Ya “Wireless Charging”!

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

‘Wireless Charging’ ni teknolojia ya kuchaji simu ambayo haihusishi chaja kuchomekwa katika simu moja kwa moja..Ili kuchaji inakubidi kuweka simu yako juu tuu ya kifaa cha kuchajia, hii inasaidia sana katika swala zima la kuokoa muda na pia simu kujaa haraka.

Katika matoleo ya simu za Samsung je ni yapi ambayo unahisi yanaruhusu teknolojia hii? Je unahisi ni matoleo yote yanaruhusu? Leo  TeknoKona inakuletea jibu au majibu ya maswali hayo.

Wireless Charger

Wireless Charger

Kwa mujibu wa mtandao wa Samsung, matoleo haya ndio yanakubali teknolojia ya ‘wireless charging’

Galaxy Note10

Galaxy Note10+

Galaxy S10e

Galaxy S10

Galaxy S10+

Galaxy Note9

Galaxy S9

Galaxy S9+

Galaxy Note8

Galaxy S8

Galaxy S8+

Galaxy S7

Galaxy S7 edge

Galaxy Note5

Galaxy S6 edge+

Galaxy S6 edge

Galaxy S6.

Inasemekana kwamba matoleo mengine ya Samsung ambayo yatakua ni ya juu zaidi ya hayo tajwa hapo juu yanaweza yakaja na teknolojia hii.

Wireless Charger

Wireless Charger

MUHIMU

Samsung hata kama inakubali teknolojia hii haitaweza kuchaji kama ukiwa umeiunganisha moja moja na chaja ya kawaida au USB. kwa kifupi unaweza kuchaji kwa kutumia chanzo kimoja kwa muda husika.

Jitahidi kuweka ‘Silent’ (bila vibration) au weka ‘airplane mode’ ili kufanya simu kuwa kimya maana baadhi ya ‘notification’ za ujumbe mfupi na mitandao ya kijamii zinasababisha simu kunguruma (vibrate) hii inaweza sababisha simu yako kuhama katika eneo lake la kuchajia.

Vile vile simu  inaweza onyesha hali ya kupata hali ujoto joto ambao sio wa kawadia. Ujoto joto huu unaweza kuwa unasababishwa na koili ndani ya ‘wireless charger’ na simu hazijarandana vizuri. Sasa ili kuepukana na hili inabidi haili hii ikitokea, uache kuchaji simu yako kwa muda au uende kuchajia katika eneo ambao ni tulivu na lenye ubaridi ubaridi (sio ubaridi kama wa jokofu) mfano karibia na feni.

Chanzo: Samsung n.k  

Kuhusu Samsung zinazokubali Wireless Charging bofya hapa

INAYOHUSIANA  WorldRemit na Huawei wawezesha miamala ya simu nje ya Afrika

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini sehemu ya maoni kama una swali lolote kuhusiana na teknolojia ya ‘wireless charging’

Tembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kila siku kwani daima tupo nawe katika sayansi na teknolojia kwa ujumla.

 

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.