fbpx

VIdeo za makundi kwenye Instagram sasa ni rasmi

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Mara kadhaa tumekuwa tukiandika kuhusu ujio wa video za makundi kwenye Instagram na watu wengi kuonekana kufurahia kitu hicho kipya sasa kipengele hicho ni rasmi kimeshawekwa.

Video za makundi/kuweza kumshirikisha mtu mwingine kwenye mazungumzo kwa njia ya picha jongefu ni kitu ambacho watu wengi walikuwa wakikiongelea na hivyo kuwafanya wale wataalamu wa kuandika programu kulifanyia kazi suala hilo.

INAYOHUSIANA  Mambo 20 Kuhusu Mtandao Wa Kijamii Wa Twitter!

Sasa ni rasmi nikiwa na maana ya kwamba mtu anaweza kuanzisha mazunguzo ya video ya zaidi ya mtu mmoja kwenye Instagram kwa kubonyeza kitufe cha kamera.

Ni takribani watu watano (5) pamoja na wewe mwenyewe ndio wanaweza kufanya mazungumzo kwa njia ya picha jongefu kwa wakati mmoja kwenye Instagram.

VIdeo za makundi kwenye Instagram

Watu wamme wakiwasiliana kwa wakati mmoja huku ikiwa bado nafasi moja kutimia watano.

Mbali na ujio huo pia, bado wahusika wameendelea kuongeza vikatuni ambavyo vimekuwa maarufu sana kwa kuongeza nakshi nakshi kwenye picha/picha jongefu.

VIdeo za makundi kwenye Instagram

Wakati huo huo ukiwa unaongea na mtu/watu unaweza ukaremba sura yako kwa urembo vikatuni vilivyoongezwa kwenye huko (Instagram).

Unafikiri ukiwa unaongea kwa njia ya picha jongefu huwezi kuperuzi?

La hasha! Bado utakuwa na uwezo wa kufanya mengine kama ilivyo kwenye kompyuta, unaweza ukaufanya ule uwanja wa mazungumzo yenu kuwa mdogo huku wewe ukiendekea kuangalia mengineyo kwenye Instagram.

VIdeo za makundi kwenye Instagram

Ukishamkubalia mtu kujiunga kwenye video ya kundi ule ukurasa utajisogeza na utaona mtu mwingine ameongezeka.

Kipengele hicho hakipo kwenye hatua ya majaribio kwahiyo kinapatikana kwenye Android na iOS, kitu cha msingi tu ni kufanya masasisho programu tumishi ya Instagram.

Vyanzo: Engadget, TechCrunch

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.