fbpx
apps

Boomplay watoa takwimu za muziki 2019: Diamond Platnumz aongoza

boomplay-watoa-takwimu-2019
Sambaza

App namba moja kwa huduma ya muziki barani Afrika, Boomplay watoa takwimu za muziki za 2019. Takwimu hizo zimemtaja msanii Diamond Platnumz, kuwa ndio mwanamuziki aliyesikilizwa zaidi Tanzania,.

Taarifa hiyo iliyowekwa kwenye ripoti maalumu kuhusu muziki imeegemea zaidi data kutoka kwenye app hiyo ya muziki ambayo ina watumia zaidi ya milioni 60, ulimwenguni kote huku Tanzania kukiwa na watumiaji zaidi ya milioni 4.2.  Boomplay inajivunia kuwa na aina tofauti za nyimbo ambazo idadi yake ni zaidi ya milioni 20, ambazo zinapatikana kwenye iOS, Android na web.

INAYOHUSIANA  Emoji mpya 2017 zinakuja, zifahamu mpya zinazokuja
Watumiaji Boomplay
App hii imefikisha jumla ya watumiaji zaidi ya milioni 62 duniani kote

App ya Boomplay inakuwezesha kusikiliza nyimbo za ndani ya Tanzania na za kimataifa bure, kwa malipo unaweza kununua wimbo mmoja mmoja, albamu nzima au kusikiliza nyimbo zozote utakazo bila kutumia intaneti (Download & Save ndani ya BoomPlay).

Nafasi ya pili imenyakuliwa na mwanadada Nandy, na ya tatu kuangukia kwake Harmonize huku Rayvanny akishika namba nne. Nae Aslay amekamata namba tano, huku namba sita ikinyakuliwa na Mbosso. Jux nae akainyakua nafasi ya saba huku Lava Lava akiijaza namba nane, mwanamuziki pekee wa injili katika orodha hii ni Joel Lwaga aliyeshika namba tisa na namba kumi akisimama mwanadada shupavu Vanessa Mdee.

INAYOHUSIANA  Baada ya siku na miezi kadhaa Apps za HTC zarudi Google PlayStore
Boomplay watoa takwimu kulingana na taarifa rami za muziki mwaka 2019
Kulingana na taarifa rami za muziki mwaka 2019, msanii Diamond Platnumz yupo juu katika huduma hiyo kwa Tanzania.

 

Boomplay watoa takwimu diamond Boomplay watoa takwimu
Boomplay watoa takwimu za mwaka 2019

Mbali na wasanii, Boomplay pia imekusanya taarifa kuhusu nyimbo ambazo zimesikilizwa zaidi pamoja na albamu, ambapo wimbo wa Diamond Platnumz akiwa na Fally Ipupa ‘Inama’ ndio umetisha zaidi kwa mwaka 2019. Albamu ya Nandy ya “The African Princess” imeshika nambari moja, huku “The Love Album” ya Jux ikishika namba mbili na kufuatiwa na “A Boy From Tandale” ya Diamond Platnumz iliyoangukia namba tatu.

INAYOHUSIANA  App ya Youtube kwenye Android imefanyiwa maboresho ili kuvutia zaidi

Boomplay pia imetoa taarifa za mwenendo na tabia za namna muziki unavyosikilizwa Tanzania. Katika taarifa hiyo maalumu, Nyimbo Za Injili (Gospel) zimeonekana kusikilizwa zaidi na kufuatiwa na miondoko ya Bongo Flava, kisha Afrobeats inashika namba tatu, huku ya nne na tano zikishikwa na Hip Hop & Rap pamoja na Reggae.

Je wewe ni mtumiaji wa app ya BoomPlay? Jiunge nami na fuatilia ‘playlists’ zangu kutafuta username – stevpm

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: , ,

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |