fbpx

Teknolojia, Usafiri

Unafahamu kuhusu Uber Connect na Uber Direct?

unafahamu-kuhusu-uber-connect-na-uber-direct

Sambaza

Uchumi duniani kote umetetereka kutoka na janga la virusi vya Corona ambavyo vimesababisha shughuli nyingi za kijamii, kisiasa, n.k kusimama ili kukabiliana na janga hilo lakini kwa namna moja au nyingine ni muhimu kutafuta mbaldala wa kupata riziki, sasa kuna Uber Connect na Uber Direct!

Hivi sasa hakuna dereva wa Uber duniani kote atakayekwambia kuwa biashara hiyo inamlipa bali ni hasara tuu au kupata kidogo kuliko vile ambavyo alikuwa akiingiza hapo mwanzo. Hata hivyo, tatizo la virusi vya COVID-19 vimeifanya kampuni ya Uber kwenye mataifa kama Marekani, Australia na Mexico kuanzisha huduma mbili za kipekee kabisa wakati huu ambao hakuna mzunguko mkubwa wa biashara.

Huduma hizo mpya ni Uber Connect na Uber Direct ambazo kila moja haziingiliani majukumu yake. Sasa, Uber Direct inatoa huduma kutoka duka la dawa, nyumba za kuhifadhia wanyama wadogo kwenda kwa mteja huku Uber Connect yenyewe ni kusafirisha mzigo kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

Uber Connect
Uber Connect: Huduma mpya ambayo inalenga kurahisisha usafirishaji wakati huu wa janga la virusi vya Corona.

Ni suala lisilopingika kwamba nchi zetu za Afrika zinahitaji mfumo huo wa usafirishaji wa bidhaa kutoka sehemu moja hadi nyingine hasa wakati huu ambapo madereva wengi wanashindwa kujipatia kipato ipasavyo kutokana na tatizo lililoikumba dunia. Je, wewe una mawazo gani?

Vyanzo: TechCrunch, The Verge

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Dropbox wadukuliwa; Mamilioni ya akaunti hatarini
0 Comments
Share

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|