fbpx

Mkazo kuhusu kutolipia chaneli za ndani

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Ukizungumza na wateja wa visimbuzi mbalimbali bado watakwambia inawalazimu kulipia ili kuweza kupata kuona matangazo ya chaneli za ndani ambapo kwa mujibu wa mamlaka husika huduma hiyo inapaswa kuwa BURE!.

Kuna baadhi ya wateja wanapata huduma ya matangazo ya chaneli za ndani ambayo yalipotea kwa kupindi fulani lakini hapohapo pindi tu kifurushi cha mwezi kinapoisha chaneli zote ( isipokuwa TBC 1) zinakata hivyo inakubidi uweke kifurushi kingine ili kuweza kurejea kupata huduma lakini hivyo si sahihi!

Katika mazungumzo na mmoja wa watu kutoka ngazi ya juu kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) akaniambia wananchi hawapswi kulipia ili kupata matangazo ya chaneli za ndani na iwapo wakitakiwa kufanya hivyo basi wapige namba maalum kutoa taarifa kwa TCRA hatimae atarudishiwa hela yake lakini pia ataendelea kuona chaneli za ndani kama kawaida.

Kilichonisukuma kutaka kupata ukweli.

Sio mara moja au mbili rafiki yangu amekuwa akiniambia kuwa analazimikia kulipia kifurushi kipya kuweza kuona matangazo ya chaneli mbalimbali zikiwemo za ndani na alipojaribu kuuliza alijibiwa “Chaneli za BURE ni kwa wale wanaotumia antena za ndani pekee“. Lakini mamlaka husika inasema huo ni ulaghai na kampuni zilishapewa maelekezo na wakakubali kurusha matangazo hayo kuendelea kuonekana hata kama kifurushi cha mteja kimekwisha.

Nafasi ya TBC 1.

TBC 1 ni runinga ya taifa ambayo kwa mujibu wa sheria duniani kote televisheni ya taifa inaapswa kuonekana bila kulipiwa pasipo kujali aina ya king’amuzi ambacho mteja anatumia na sababu kuu ikiwa ni mwanachi aweze kupata habari/taarifa zinazoendelea nchini kwake hata kama kisimbuzi chake kina salio au la!.

 kutolipia chaneli

Chaneli mbalimbali zinzopatikana kwenye king’amuzi cha Startimes ambao wanaongoza kwa kulalamikiwa na wateja wao.

TeknoKona kwa nafasi yake imeweza kutafuta ukweli kuhusu  kutolipia chaneli sasa sehemu iliyobaki ni yako wewe mwananchi ambae unakumbana na kadhia hiyo kila mwezi. Piga simu namba +255737300300 kuweza kutoa malalamiko yako.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Simu imepotea tuma IMEI kwenda cop@vsl.net - Hii habari ni ya uongo, usifanye hivyo
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.