Google wanaendelea na kongamano lao la Google I/O wanalofanya kila mwaka na katika waliyotangaza rasmi ni pamoja na ujio wa apps za Android kwa watumiaji wa programu endeshaji yao ya Chrome OS. Fahamu mapya ktk Android na mengine mengi.
Hii ni moja ya habari kubwa na iliyowafurahisha wengi kwani tayari laptop zinazotumia programu endeshaji hiyo zinafanya vizuri sana sokoni na inategemewa zitaendelea kuuzika sana.
Tayari programu endeshaji ya Chrome OS ina apps nyingi lakini bado watengenezaji apps za uhakika zisizohitaji uwepo wa intaneti hawakuwa wametengeneza apps nyingi za kutosha na hivyo uamuzi wa kuweka uwezo kwa Chrome OS kutumia apps za Android umeonekana ni uamuzi bora sana na ambao utafanya ata watengenezaji apps kuvutiwa zaidi. Kwani sasa wanatakuwa na watumiaji wengi zaidi, kuanzia simu, tableti hadi kompyuta kupitia Chrome OS
Vingine vilivyotambulishwa katika kongamano la Google I/O
Android N: Toleo lijalo la Android
Wametambulisha toleo jipya la Android litakalokuja baada ya la sasa la Android 6.
Ingawa bado jina lake kamili halijatambulishwa, Android N, ina maboresho makubwa ya kasi na ya kimuonekano. Tegemea matumizi madogo ya chaji ukilinganisha na matoleo ya sasa. Maboresho mengine ni pamoja na uwezo wa programu endeshaji hiyo kucheza vizuri magemu kutokana na maboresho yaliyofanyika kwa jinsi Android N inatumia ‘3D Graphics’.
Pia kuna uwezo ambao utaletwa kwa watumiaji wa Android (inaonekana utaletwa hadi kwa matoleo ya nyuma) baadae mwaka huu – tumia/jaribu apps bila kuzipakua (install) kwenye simu yako.
Waja pia na apps za kuchat, Allo na Duo.
Allo ni app ya kuchati ambayo inaendeshwa na ‘AI’ (Artificial Intelligence). Kama vile ilivyo Whatsapp na app zingine za kuchati app hii itaitaji namba yako ya simu kutengeneza akaunti, pia utakuwa na chaguo la kuunganisha na akaunti yako ya Google.
Kwenye Allo utaweza kuchati na watu kama ilivyo kwenye WhatsApp, ikiwa ni pamoja na utumiaji wa Emoji, stika mbalimbali na ata pia kuchora juu ya picha mnazotumiana.
Tofauti kubwa katika Allo ni utumiaji wa teknolojia ya Google Assistant ndani yake. Kupitia Google Assistant utaweza kuuliza mambo mbalimbali ndani ya app hiyo na utapatiwa majibu – yawe kutoka mtandaoni n.k. Pia unaweza ruhusu uwezo wa Google Assistant kukusaidia kuandika majibu ya meseji unazopokea.
Sifa zingine
- Meseji zote zipo salama, teknolojia ya ulinzi ya encryption inatumika.
- Pia uwezo wa meseji zinazojifuta baada ya muda upo pia
WhatsApp, Facebook Messenger, SnapChat n.k Je unafikiri tunaitaji kweli app nyingine kwa ajili ya kuchati?????
Duo, app hii ni mshindani kwa app ya Apple iliyokwenye simu za iPhone ya FaceTime
Duo ni app ya kuchati kwa simu za video. Tofauti kuu ni kwamba Google wamejitahidi kuifanya iwe ni rahisi sana kutumika.
Ukiifungua tuu unakutana na video ya wewe kupitia kamera ya selfi.. kisha utaweza chagua mtu unayempigia, anayepigiwa atapata muda wa kukuona pia ata kabla ya kupokea.
App ya Duo nayo inaitaji namba yako ya simu tuu kujiandikisha, na itapatikana kwa watumiaji wote, wa iOS na wa Android.
Google Home
Wamekuja na kifaa unachoweza kukiita msaidizi wa nyumbani, ‘Home assistant’. Kupitia kifaa cha Google Home ambacho kina sifa ya kuwa spika janja (smart speaker) utaweza kupata taarifa mbalimbali muhimu kutoka simu yako uliyounganisha nacho. Pia badala ya kuingia kwenye simu kutafuta juu ya jambo utaweza tuu kuiuliza Google Home nacho kitakujibu.
Kwa ufupi Google Home ni roboti-spika, kwa kutumia data zako za Google utaweza kupatiwa taarifa za hali ya hewa, kufanya booking ya vitu kama Sinema n.k. Ufanyaji kazi wake unategemea pia teknolojia ya Google Assistant.
Je ni kipi kimekuvutia katika haya? Tutaendelea kukupa habari mpya kutoka kongamano la Google I/O
Vyanzo: TheVerge na mitandao mbalimbali