fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Teknolojia

Pavlok: Inakupiga “shoti” ya umeme pale unapofanya matumizi mabaya ya pesa

Pavlok: Inakupiga “shoti” ya umeme pale unapofanya matumizi mabaya ya pesa

Spread the love

Kampuni moja ya nchini Uingereza inatarajia kuweka kifaa kinachodhibiti matumizi ya pesa kwa kuwapatia wateja wake mshtuko wa umeme iwapo watapitisha kiwango cha matumizi yao (budget).

pavlok

Mpira wa kuvaa mkononi uliopew jina la Pavlok

Kampuni ya “Intelligent Environments” imezindua mfumo ambao utaiunganisha na mpira (lastic) wa kuvaliwa mkononi (wristband) wa “Pavlok” ambao unatoa mshtuko wa volti 255 – 340 za umeme pale taarifa ikizifikia ya kwamba umetumia pesa kinyume na mipango yako.

Kiasi hicho cha umeme hakitakuua ila lazima utasikia maumivu yake kiasi

Pia mpira huo una uwezo wa kufanya kazi na mita za umeme (luku) kuzuia matumizi ya juu ya umeme na kuokoa bili iwapo fedha hizo zitashuka, na pia ata kuunganishwa na bili zingine zinazofanywa kwa matumizi ya kadi za benki.

Mtendaji mkuu wa kampuni “Intelligent Environments” Bw. David Webber alisema wazo hilo lilikuwa kwa mapendekezo ya wateja.

New tech

Mteja akijaribu kutoa pesa kwenye ATM

Watumiaji wa Pavlok wataweza kuweka taarifa zote muhimu za kibajeti kupitia app ya wristband hiyo inayopatikana kwenye simu. Mtumiaji atajiwekea kiwango cha matumizi yake mbalimbali na pia kuomba kupata taarifa za mara kwa mara (alerts) kuhusu hali ya kibajeti na pia kiwango cha shoti ya umeme cha kupewa pale wanapoenda kinyume na bajeti hiyo.

SOMA PIA  Maujanja ya kivinjari cha Google Chrome

Intelligent Environments wanafanya biashara ya kutengeneza teknolojia mbalimbali za kibenki lakini bado hawajapata benki iliyo tayari kwa sasa kutumia teknolojia hii.

Vipi mtazamo wako, unadhani teknolojia kama hii itakusaidia katika kusimamia matumizi yako?

Chanzo: Pavlok.com

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania