fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Teknolojia

Firefox OS : Sahau Kuja kwa Simu Janja za Elfu 50!

Firefox OS : Sahau Kuja kwa Simu Janja za Elfu 50!

Spread the love

Kama ni mfuatiliaji wa muda mrefu wa mtandao wako wa TeknoKona basi utakuwa umeshakutana na habari kuhusu uhamuzi wa kampuni ya Firefox kuja na programu endeshaji iitwayo Firefox OS kwa ajili ya simu na tableti. Lengo kuu lao lilikuwa kuweza kufanikisha programu endeshaji hiyo kutumiwa katika simu zitakazokuwa zinauzwa kwa bei rahisi sana, hii ikiwa ni dola 25 za kimarekani au takbribani Tsh 50,000 za kitanzania.

Wameshafanikiwa kutoa matoleo kadhaa hasa kwenye nchi za amerika kusini na tayari baadhi ya makampuni yalianza kufikiria kutengeneza simu za Firefox OS kwa ajili ya soko la Afrika. Uongozi wa Firefox umekiri ya kwamba ni vigumu kufanikiwa katika eneo la programu endeshaji ya simu kama wakifikiria kutoa simu za bei rahisi tuu. Wamegundua ya kwamba watu wengi wapo tayari kulipa zaidi ili kupata simu zenye ubora na uwepo wa apps zao mbalimbali wanazozitumia kila siku. Ni vigumu kumuambia mtumiaji anunue simu ya Firefox OS ya Tsh 50-80 wakati kama akiongeza pesa kidogo anaweza kupata simu yenye Android na yenye uwezo wa kupata apps chungunzima kulinganisha na Firefox OS ambayo bado ni changa.

Muonekano wa simu inayotumia Firefox OS iliyotengenezwa na kampuni ya ZTE
Muonekano wa simu inayotumia Firefox OS iliyotengenezwa na kampuni ya ZTE

Firefox Foundation ni shirika lisilo la kifaida (Non-for-profit) linalojihusisha na utengenezaji na usimamiaji wa maendeleo ya kivinjari ya Firefox na teknolojia zingine mbalimbali kama vile Firefox OS.

Kuanzia sasa kampuni hiyo inajipanga katika kuleta simu zenye kiwango kizuri cha kuweza kumvutia mnunuaji, suala la bei litakuwepo lakini sio kipaumbele tena. Kipaumbele ni kuboresha zaidi Firefox OS na pia kuleta sokoni simu zenye kiwango kizuri. Kimombo mkurugenzi wa shirika hilo amesema wata-focus on quality over others – affordability etc’, yaani kwa sasa ubora ndio utapewa kupaumbele zaidi ya maeneo mengine kama vile suala la bei.

Inazidi kuonekana ya kwamba ni vigumu sana kwa programu endeshaji mpya kujitokeza na kukua, wanunuaji simu wengi wanataka simu za Android na iOS tuu

Wengi wanaona ni vigumu sana kwa kampuni hiyo kufanikiwa kwa sasa. Firefox OS inaonekana imechelewa kuja sana kwani tayari soko limeshikiliwa sana na iOS na Android. Ata kwenye eneo la vivinjari vinavyotumika zaidi katika simu Opera Mini inatumika zaidi ya ata kivinjari cha Firefox kutoka shirika hilo.

SOMA PIA  Magemu ya video yaruhusiwa tena Uchina

Je kwa mtazamo wako unafikiri kuna uhitaji wa programu endeshaji nyingine kwenye simu zaidi ya Android, iOS na Windows?

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Comments

  1. julius philipo - May 26, 2015 at 18:20 - Reply

    Ni maamzi ya msingi sana n bora waiboreshe .. sisi tunaisubili.. ifike afrika tununue

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania