fbpx

Ondoa vitu kwenye Thumbnails kuongeza nafasi

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +

ICT CONFERENCE 2019

Sambaza

Kwenye simu zenye kutumia mfumo endeshi wa Android kuna faili moja linafahamika kwa jina la Thumbnails ambalo linakuwepo ndani ya simu na wengi wa watumiaji wake pengine hawajawahi kuliona au kutokujua kwanini lipo ndani ya simu zao.

Kupitia hapa teknokona tutakufahamisha kwa ufupi kazi yake ndani ya simu yako. Kazi yake nini? Thumbnails kazi yake ni kuhifadhi picha zote ulizowahi kuzingua kwenye simu yako. Hii ni kukurahisishia namna ya kuzipata picha zote ulizofungua.

Picha/video yoyote uliyoiweka ndani ya simu au kuipiga na kuanza kuifungua kwa kuiangalia basi itahifadhiwa kwenye faili hili maalum la Thumbnails hivyo kusababisha kuchukua nafasi (kujaza) memori ya ndani ya simu.

Kwa lugha nyingine  zinakuwa zimehifadhiwa mara mbili-mbili; sehemu ya kwanza kwenye Gallery na kwenye Thumbnails (kwa zile ulizozifungua).

Je, inawezekana kulifuta? Ndio, inawezekana kulifuta na kusiwe na madhara yoyote kwenye simu yako. Unapofuta faili la Thumnails itakusaidia sana kurudisha nafasi kwenye simu yako ambapo utaweza kuingiza au kuhifadhi vitu vingine.

Namna ya kulifuta faili la Thumbnails kuna njia kadhaa ikiwemo ya kutumia Programu maalum kama CCleaner, Clean Master  na nyinginezo. Fuata njia hii kuondoa vitu vyote kwenye Thumbnails bila kutumia programu yoyote:

My files/File Manager>>Settings>>Hidden files (weka alama ya pata)>>Device storage>>DCIM>>.thumbnails. Bonyeza kwa ujula na kisha bofya delete kuweza  kuondoa zile picha/video ambazo tayari zipo sehemu nyingine ila zipo huko kwa sababu ulizifungua.

kuongeza nafasi

Kama hukuliona hakikisha umeruhusu kipengele cha “Show hidden files”.

Simu kuwa na nafasi ni jambo zuri na kusaidia sana kwenye ufanisi wake wa kazi, ifanye simu yako kuwa nyepesi kwa kutohifadhi vitu ambavyo havina ulazima kuwepo.

Facebook Comments

Sambaza

ICT CONFERENCE 2019

INAYOHUSIANA  Njia 3 Za Ku 'Reset' Simu Ya Android!
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.