fbpx

VPN ni nini? Fahamu app 3 za bure za Huduma ya VPN

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +

ICT CONFERENCE 2019

Sambaza

Intaneti ni kiungo muhimu sana katika ulimwengu wa teknolojia katika kuwezesha mambo mbalimbali ambayo yanahitaji kuwasiliana lakini kuna wakati inabidi mawasilano hayo yafahamike kwa kundi fulani tu la watu na ndio VPN inapokuwa muhimu sana.

VPN (Virtual Private Network) ni nini? VPN ni muundo wa mtandao kwenye intaneti ambao unafanya kundi au kampuni tu ndio wawe na uwezo wa kuutumia aina hiyo ya mawasiliano.

Intaneti inayotolewa mathalani na Smart Tanzania inaweza ikawa inatumiwa na watu wengi lakini kampuni fulani inatumia chanzo hicho isipokuwa wenyewe wana mtandao mdogo ambao hauingiliwi na wengineo wanaotumia intaneti ya Smart Tanzania.

VPN ni nini

Benki zote huwa zinatumia teknolojia ya VPN ili kulinda usalama wa mawasilano yao.

Mfano mwingine dhahiri ni pale sheria ya kodi kwenye mitandao ya kijamii ilipoanza kutumika rasmi Julai Mosi ndipo watu wakaona mbadala ni kutumia VPN ili kukwepa kulipa kodi hiyo. Kusoma zaidi>>BOFYA HAPA.

Programu tumishi bora za kutumia kwenye simu.

Sasa kwenye simu kama hutaki watu mbalimbali wajue unachofanya inakubidi utumie VPN lakini swali linabaki kuwa ni programu tumishi zipi za VPN ni nzuri?

INAYOHUSIANA  Kukosea namba ya mtu anayempigia kwamuwezesha msichana kupata mume

OpenVPN Connect. Hii ni programu tumishi ya bure kabisa ambayo hutahitaji kuilipia na itakuwa inafanya kile ambacho ilitengenezwa ikifanye. Playstore|OpenVPN Connect.

VPN ni nini

Muonekano wa programu tumishi ya OpenVPN Connect.

Proton VPN. Haina ukomo wa kuitumia na hutalipia gharama yoyote ili kuweza kuitumia bila kusahau kufanya kasi ya intaneti iongezeke. Kuweza kuipakua>>Proton VPN BOFYA HAPA.

VPN ni nini

Huo ndio muonekano wa Proton VPN.

Speed VPN. Hii ni programu tumishi nyingine ambayo unaweza kuipakua kwenye simu yako ya Android na kuwa salama kwa wale ambao wanapenda kufuatilia na kutaka kujua unachokifanya mtandaoni. Ingia>>HAPA KUIPAKUA.

VPN ni nini

Speed VPN inakuwa uwezo wa kuchagua kuunganisha/kuatisha ktumia VPN muda wowote utakaotaka.

Maamuzi ni yako sasa kuamua kushusha moja kati ya hizo tulizoziainisha na kuzitolea maelezo au kuingia kwenye soko husika na kuchagua utakayoipenda. Usisite kutuandikia maoni yako hapo chini.

Vyanzo: Android Authority, mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza

ICT CONFERENCE 2019

Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.