fbpx

Teknolojia

Apple kuanzisha Academy, kufundisha wanafunzi kuhusu utengenezaji apps katika iOS

apple-kuzindua-academy-kufundisha-ios

Sambaza

Apple waungana na chuo kikuu cha Naples Federico II kuanzisha Academy (chuo cha mafunzo) kwa ajili ya waundaji wa iOS iliyochini ya Apple na kuzinduliwa mwezi Oktoba.

Apple waungana na chuo cha Naples kuanzisha academy kufundisha wanafunzi jinsi ya kutengeneza iOS
Apple waungana na chuo kikuu cha Naples kuanzisha academy kufundisha wanafunzi jinsi ya kutengeneza iOS.

Takribani wanafunzi wapatao 200 watapata nafasi ya kuweza kujifunza jinsi ya kutengeneza apps kwa ajili ya programu endeshaji ya iOS inayotumika kwenye simu za iPhone na tableti za iPad. Mafunzo hayo yatadumu kwa zaidi ya miezi 10 ambapo yatashirikisha wataalamu kutoka Apple na chuoni hapo kuweza kuwafundisha wanafunzi hao.

Katika muhula wa kwanza wanafunzi wataweza kuongeza msukumo wa jinsi ya kuweza kutengeneza programu/apps kwenye iOS. Katika muhula wa pili wanafunzi hao wataenda mbali zaidi ya uundaji(coding) na kuweza kujua jinsi ya kuunda muonekano wa awali wa programu hiyo endeshaji.

Wanafunzi watakuwa wanajifunza katika makundi na binafsi (individually) na kutengeneza apps mbalimbali ambazo zitawekwa kwenye ‘App store’. App store inatoa ajira zaidi ya 75,000 nchini Italia, kwa hakika idadi hiyo itaongezeka baada ya wanafunzi hao kuhitimu mafunzo yao.

INAYOHUSIANA  Waliopewa dhamana ya kusimamia mifumo ya TEHAMA serikalini waonywa na kutakiwa kuzingatia weledi kazini
Chuo cha Napoli, Italia.

Ingawa Apple hawajasema ni nchi gani itakayofuata kuweza kuwa kuwa na academy kwa ajili ya kufundisha wanafunzi jinsi ya kutengeneza iOS, nchini India Aoole wana mpango wa ‘kudesign’ na kujenga kituo Hyderabad kitakachokamilika mwaka 2017.

Wanafunzi ambao watapenda kujiunga katika academy hiyo wanatakiwa kutuma maombi yao katika tovuti yao chuo na ni bure kwa wanafunzi kutoka bara la Ulaya. Scholarships zipo kwa baadhi ya wanafunzi na itajumuisha pesa kwa ajili ya kuweza kujikimu. Waombaji wote watapewa jaribio(test) ambayo itakuwa katika lugha za Kiingereza na Kitaliano.

INAYOHUSIANA  Xiaomi yaendelea kukua kwa kasi

Kwa mtu yeyote amabye angepnda kujiunga na programu hiyo itakayoanza mwezi wa 10 kwa ajili ya kufundisha anaruhusiwa kujiunga kupitia academy ya waundaji wa iOS.

Je, unadhani hii ni mbinu tu ya Apple kujipatia developers kiulani? Tuambie mawazo yako katika comment. Teknokona siku zote tunakuletea makala za kusisimua.

Vyanzo: Tech, times, MacRumors.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Sambaza

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|