Kuamka. Ni neno la herufi chache ila ni kitendo ambacho ukichelewa kukifanya kulingana na mipango yako kinaweza kikakugharimu sana. Kuna kipindi ambacho watu wengi walikuwa wananunua kengere ila ukweli ni kwamba siku hizi simu zetu zimekuwa zikitumika zaidi katika suala lote la alam hasa kutuamsha.
Zifuatazo ni app muhimu za kengere, kimombo ‘alarm’ kwa ajili ya watu wa aina zote, wale wanaoweza amka haraka baada ya mlio, na kwa wale ambao huwa wanaminya ‘snooze’ haraka na kuendelea kulala.
Wave Alarm
App ni nzuri kwa watu ambao hawaitaji kujivuta sana kuamka. Wave Alarm inatumia kamera ya mbele ya simu au tableti kukuwezesha kuzima alam au kusogeza mbele (snooze) kwa kupunga mkono wako tu. Kupitia ‘settings’ unaweza kuchagua kama unaitaji iwe inazima kabisa au kusogeza muda mbele pale ukiipungia mkono. Wave Alarm inamuonekano mzuri na inaonesha muda, tarehe na habari za hali ya hewa.
Kushusha kwenye simu yako bofya hapa! (bure)
Alarm Clock Extreme
Alarm Clock Extreme ni muhimu kwa wenye huitaji wa msaada zaidi katika kuamka. Inakupa uhuru mwingi zaidi katika mfumo mzima wa sauti, kelele na jinsi gani muda wa alam usogezwe mbele(snooze) au kuzima. Unaweza kutoa kabisa chagua la kusogeza mbele hivyo alam ikiita hauna jinsi ni kuizima moja kwa moja tu. Pia katika kuzima au kusogeza mbele muda unaweza kuchagua iwe kwa mfumo gani kama ni kwa kutingisha simu, kutatua mahesabu ambayo yapo kwa ugumu mbalimbali au kwa kujaza ‘kaptcha’ (yale maneno yanayoandikwa ovyo na kuwa na uwezo wa kukuchanganya usipotazama kwa umakini zaidi).
Kushusha kwenye simu yako bofya hapa! (bure)
I Can’t Wake Up!
Kama wewe ni mzito linapokuja suala la kuamka basi ‘I Can’t Wake Up'(KSw-Siwezi Kuamka) app ni kwa ajili yako. Kama hesabu ndogo haziwezi kukuamsha bado basi hii ndio alam kwa ajili yako. Hii ni kuja na michezo tofauti 8 ya kukusaidia kuamka. Kuna michezo inayohusu kumbukumbu, kutikisa simu kwa muda fulani hadi eneo la duara libadilike rangi na mingine mingi migumu ya kukufanya usingizi wote uondoke.
Kushusha kwenye simu yako bofya hapa! (bure)
Hizo ndio moja ya apps maarufu linapokuja suala la alamu/kengere kwa watumiaji wa Android. Usisahau kushea makala hii kwa wangine na kutuandikia mchango wako
No Comment! Be the first one.