fbpx
Barua pepe, Gmail, Google, Maujanja, Teknolojia

Jinsi ya kuweka au kutumia saini kwenye Gmail

jinsi-ya-kuweka-au-kutumia-saini-kwenye-gmail
Sambaza

Katika njia mojawapo ya kufanya mawasiliano na mtu yeyote na popote duniani ni kwa kutumia na barua pepe. Mbali na hilo matumizi ya simu janja ama vifaa vya kidijiti linafanya mtu aweze kutuma jumbe kwa urahisi na haraka zaidi.

Kutokana na ukuaji wa teknolojia ambapo mtu anaweza akawa anatumia barua pepe (Yahoo, Hotmail, n.k) tofauti na Gmail lakini uwepo wa simu janja hasa za Android zimelazimisha watu kuwa na akaunti kwenye Gmail. Na ukiwa kama mtu ambae unatumia barua pepe kufanya mawasiliano mara kwa mara, kuifanya ionekane kuwa nadhifu na rasmi ni muhimu ukafahamu jinsi ya kutumia ama kuweka saini kwenye akaunti yako ya Gmail.

INAYOHUSIANA  Fahamu mfumo mpya usajili wa laini za simu

Fuata njia hii kuweza kuweka saini kwenye barua pepe (Gmail)

>Hatua ya kwanza kabisa ni kuingia kwenye akaunti yako ya Gmail kisha nena kwenye mpangilio (settings) kisha bofya “See all settings“. Kuna ukurasa mdogo utafunguka sasa shuka shuka chini mpaka utakapoona neno “Signature” halafu bofya “Create new“.

kutumia saini
Hatua ya awali kutengeneza saini ya kuambatanisha kwenye barua pepe.

>Andika jina unataka kuita faili ambalo ndani yake ndio utaweka vitu ambavyo vitasimama kama saini yako kwenye barua pepe. Kumbuka: Jina hili linaweza kuwa barua pepe ama neno lolote utakalopenda kuweka. baada ya hapo bonyeza “Create“.

INAYOHUSIANA  Simu Janja 'Phantom 9' Kutoka TECNO Hii Hapa!
kutumia saini
Sehemu ya kuandika jina la faili linalobeba saini ya mhusika.

>Sasa andika vitu ambavyo unataka saini yako iwe navyo kwa maana ya kwamba inaweza kuwa jina lako, cheo, anwani, tovuti, n.k. Vilevile, inawezekana kuweka picha ya kitu chochote. Hapa utabonyeza sehemu ya kuambatanisha picha (images).

kutumia saini
Sehemu ya kuweka picha/nembo kwa ajili ya kuwa sehemu ya saini.

>Ili kuweza kufanya saini iweze kuonekana ni lazima uchague ionekano wakati gani na kwenye akaunti ipi (kama unatumia barua pepe ambazo zote unazitumia kupitia Gmail). Baada ya hapo shuka chini kabisa na bofya “Save changes“.

INAYOHUSIANA  Google kupigwa faini ya kuvunja rekodi barani Ulaya
Muonekano wa saini kwenye barua pepe ndani ya Gmail.

>Inawezekana kutengeneza saini nyingi tuu na kuzipa majina tofauti tofauti na kuzitumia kadri ambavyo utakuwa umechagua ipi ya kutumia kwa wakati huo.

kutumia saini
Ruhusu na chagua saini ipi ya kutumia kwenye Gmail.

Kwa maelezo hayo nina hakika kabisa utaweza kufanya kila mara utakapokuwa unafanya mawasiliano kwa njia ya barua pepe. Tunakaribisha maoni yenu wasomaji wetu.

Chanzo: Mail Signatures

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|