fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
apps Intaneti Kompyuta Maujanja Mtandao wa Kijamii Spotify Teknolojia

Tinder inashirikiana na Spotify kuzindua kipengele kipya cha ‘Music Mode’

Tinder inashirikiana na Spotify kuzindua kipengele kipya cha ‘Music Mode’
Spread the love

Tinder inashirikiana na Spotify kuzindua kipengee kipya cha “Music Mode” ambapo mtumiaji atasikia wimbo uliochaguliwa na mtu kwa sekunde 30 wakati wa kuangalia wasifu wa huyo mtumiaji. Ikumbukwe kuwa Tinder na Spotify walishirikiana kwa mara ya kwanza mwaka 2016 ili kuzindua kipengele cha Wimbo, ambacho kinaruhusu watumiaji kuongeza muziki kwenye wasifu wao.

Ujumuishaji huu wa hivi punde ni njia mpya ya watumiaji kugundua nyimbo wanazopenda zinazofanana. Tinder ni mtandao wa kijamii maalum kwa ajili ya kutafutia mpenzi au mchumba mtandaoni. Watumiaji hujaza taarifa zao kama jina, picha na wasifu wao mfupi ukiambatana na orodha ya vitu wanavyopenda.

Tinder inashirikiana na Spotify

Picha: Muonekano wa App ya Tinder

‘Music Mode’ itatolewa kwa watumiaji wa Tinder duniani kote, katika masoko yote ambapo Spotify inapatikana, kwenye wiki zijazo. Kipengele kipya kitapatikana kwenye ukurasa wa “Explore”. Tinder inabainisha kuwa kipengele kipya kinatokana na mahusiano ya asili kati ya muziki na miunganisho ya binadamu kwa kuruhusu watumiaji kuunganishwa kupitia ladha zao katika muziki.

SOMA PIA  Tetesi: iPhone na iPads za Zamani Kupata Toleo Jipya la iOS 9

Kampuni hiyo inasema takriban 40% ya watumiaji wa Gen Z Tinder tayari wameongeza Nyimbo kwenye wasifu wao na wanapofanya hivyo, wanaona karibu ongezeko la 10% la muendano.

Chanzo: Engadget na vyanzo vingine.

Endelea kutembelea tovuti yetu uweze kufahamu zaidi kuhusu teknolojia na matumizi yake na pia kupata habari mbalimbali za kiteknolojia. Soma makala zetu zinginje hapa.

Semu Msongole

Digital Marketing Strategist, Content Writer, and Social Media Manager at Teknokona Blog.

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania