Kufuatia tukio la utekwa kwa mfanyabiashara Mohamed Dewji, Mkuu wa mkoa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda amesema sasa wana mpango wa kufunga kamera za CCTV katika jiji hilo.
Umefika wakati wa Mkoa wa Dar es Salaam wote kufungwa kamera za CCTV kwani hilo litaongezea weledi kwa jeshi la Polisi katika kufanya kazi zake za kukamata wahalifu.
CCTV ni kamera zinazorekodi matukio yote yanayoendelea katika sehemu ilipofungwa pamoja na ya kuyahifadhi kwa ajili ya matumizi ya pale yanapohitaji na wahusika.
