Ripoti mpya zaidi kutoka vyombo vya habari vya Korea Kusini vinasema huenda Kampuni ya Samsung ikaondoa sehemu ya kuchomekea spika za masikioni (earphone jack) katika simu zake za matoleo yajayo.
Taarifa hizo zinasema huenda Samsung Galaxy Note 10 ikawa ndio simu ya kwanza kutoka kampuni hiyo kutokuwa na sehemu hiyo. Hakuna sababu zilizotajwa kwanini Samsung inachukua hatua ya kuondoa kitu hicho kwenye simu zake, lakini ripoti inasema kwa familia ya simu za ‘S’ inaweza kusubiri mpaka kufikia toleo la Samsung S11.
Earphone/Headphone jack ni ile sehemu yenye tundu la kuingizia spika za masikioni kwa ajili ya kusikilizia muziki masikioni au kuchomeka Spika kwa usikivu mkubwa zaidi.
Kuondolewa kwa sehemu ya kuchomekea spika za masikioni kutasababisha nafasi yake kuchukuliwa na USB Type-C.
Taarifa hii ya kuondolewa kwa sehemu ya kuchomeka spika za masikionu kwa matoleo yajayo ya Samsung imepokewa kwa namna tofauti na wapenzi wa simu hizo; kuna ambao hawakufurahishwa na uamuzi huo na wapo wanaoona ni sawa kufanya hivyo.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.