fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Google Intaneti Teknolojia

Una Njaa? Tegemea Ku order Na Kupokea Chakula Kupitia Google Search!

Una Njaa? Tegemea Ku order Na Kupokea Chakula Kupitia Google Search!

Spread the love

google menu

Wale ambao waliotaka kula iliwa bidi waende kwenye website ya kampuni au wapige simu ya kampuni hilo ili waletewe chakula.  Sasa Google inakuja kutuokoa tena  kwa

kutangaza kuwa sasa watu wataweza kuagiza chakula moja kwa moja  kwa kutumia google search.

Ukiwa unatafuta migawa ya karibu (nearby restaurants) katika simu yako utaona chaguo la kuweka order (Place an order) katika majibu, Bofya hapo na chagua ungependa chakula chako kikufikie vipi.

SOMA PIA  Google yailipa Apple mabilioni ya dola kwa ajili ya kuonekana kwenye Safari

 

Jinsi inavyofanya kazi ni kwamba mtumiaji wa simu anapoamua kutafuta mgahawa ambao unatoa huduma ya kutuma chakula kwa wateja wake katika Google, Google wataongeza chaguo la  ‘Place an order’ ambapo mteja anaweza akaamua kupa click na kisha kuchagua  jinsi anavyotaka chakula chake kumfikia kisha atafungiwa na kutumiwa

Google-Search-food-orders

Kwa sababu ya hii kitu google inashirikiana na makampuni mengi ya kutoa huduma ya usafirishaji ili kukamilisha zoezi hili. Kwa sasa watumiaji wanaweza kuweka order zao katika migahawa ambayo inatumia huduma za usafirishaji kama vile Seamless, Grubhub, Delivery.com, Eat24, BeyondMenu, na  MyPizza.com tuu.

SOMA PIA  Google Jamboard: Ubao janja wenye ukubwa wa inchi 55

Hata hivyo Google inasema inajitahidi kushirikiana na makampuni mengi haraka iwezekanavyo na sio hivyo  tuu huduma hii inapatika sasa katika simu tuu.  Na pia huduma hii inapatika US tuu kwa sasa  lakini inaonekana kampuni  itaongeza Inchi nyingine nyingi tuu.

Google imekua ikiongeza taratibu taratibu utendaji wa kazi wa ‘Search’. Google Now ina uewezo wa kumsaidia mtu kufanya vitu vingi sana ukiachana na ile progamu maarufu ya Apple, Siri hata na Cortana ya Microsoft.  Wengi wanasema Google Now ndio msaidizi pekee wa mtu kwa sasa katika mtandao.

SOMA PIA  Barua ya wazi: Ni miaka tisa sasa Android mpenzi!

Kama Tanzania ikiongezwa kama nchi nyingine ambapo huduma hii itafika basi tarajia kuagiza Ugali, dagaa na kisamvu katika mgahawa wako pendwa. Pia tuambie mawazo yako juu ya huduma hii, Google wamepiga hatua?

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania