fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Teknolojia

Simu Yako Haiwezi Kukupa Saratani

Simu Yako Haiwezi Kukupa Saratani

Spread the love

Katika mazingira ya sasa ambapo karibu kila kitu na kila sekta mambo yanaendeshwa kwa teknolojia ya mawasiliano kwenye simu, kompyuta, tabiti, saa, miwani, nguo na hasa tunapotazamia kila kitu hivi karibuni, haishangazi kwamba mara kwa mara watu wanajitokeza kuonesha hofu juu ya athari za kiafya za vifaa hivi na hata kuzihusisha na kansa (Saratani).

Kwa muhtasari tu, wanasayansi na wataalamu wa afya duniani wanakubaliana kwamba hakuna utafiti uliofanikiwa kubainisha wazi jinsi simu na vifaa vingine vya kielektroniki vinavyotoa mionzi vinavyohusiana na saratani kama ambavyo watu wa kawaida wamekuwa wakihofia.

Mionzi

Teknolojia yetu ya mawasiliano ya sasa inahusiana sana na mionzi – vitu visivyoonekana kwa jicho la binadamu na hata kuhisiwa. Vifaa vyetu hivi vyote, simu, tabiti, saa-janja, hedifoni zisizo na waya, luninga, redio za FM na AM vyote hutoa mionzi ya ‘bluetooth’, wayalesi, LTE na microwave, waya za umeme na hata DUNIA na JUA lenyewe linatoa mionzi!

Suala la muhimu kutambua ni kwamba, mionzi yote haiko sawa na kuna baadhi ya njia za kuzitofautisha na ya muhimu zaidi kwenye mada hii, husika na kichwa cha habari hapa juu ni ‘ionization’ – yani uwezo wa mionzi kutoa elektroni kwenye atomu – ambayo ni chembe chembe inazotengeneza chochote chenye uhai na kisichokuwa na uhai.

Kuna ‘ionizating radiation’, yani mionzi inayoweza kutoa elektroni kutoka kwenye atomu na ‘non-ionizing radiation’, yani mionzi isiyoweza kufanya hivyo.

Celli za Mwili

Kwenye sayansi, kama atomu moja ikipoteza elekroni, haina shida kwani itaweza kushirikiana na atomu nyingine kuipata ‘balance’ yake ya elektroni. Binadamu, kwa upande mwingine, anatengenezwa na atomu nyingi zilizofungamana (molecule) na zenye ushirikiano wa kikemikali zaidi ya atomu zilizo kivyakevyake. Elektroni zikitenganishwa kutoka kwenye moleculi, vitu mwilini huacha kufanya kazi kama vinvyotakiwa.

SOMA PIA  Google Play Store Ya Kwenye Kompyuta Yapata Muonekano Mpya!

Kuna moleculi moja ambayo ikiharibiwa na ‘ionzing radiation’, shida kubwa itazuka mwilini. Moleculi hiyo ni muhimu katika kutoa muongozo wa jinsi celli zinavyofanya kazi na inaitwa DNA (deoxyribonucleic acid). Wakati Celli inajigawa – kitu ambacho kinatokea kwa kawaida karibu mara trillioni mbili kwa siku ndani ya mwili wa binadamu, DNA inajigawa sawia kwa kila celli itakayotokea hapo. Na wakati yai linapo-ungana na celli ya mwanaume, nusu ya kodi kutoka kila celli hungana kutengeneza kodi mpya – binadamu mpya.

DNA na Mionzi

Kuna uwezekano saa nyingine, kwamba mambo yakaenda kinyume na yanavyotakiwa kwenye kugawanyika kwa celli na hapo ndipo kunaweza kutokea celli isiyo na uhai (dead cells) ambayo inajiunga pamoja na celli zingine mfu kutengeneza ngozi na hatimaye kutoka nje ya mwili au katika maana ya uzazi, kizazi kisicho na uhai. Kuna mara chache sana, katika mchakato huo huo, zinatokea celli ambazo siyo mfu ila hazifanyi kazi vizuri. Hapa ndipo anapozaliwa mtu mwenye upungufu au inapoanza kansa (saratani).

Hatahivyo, mara nyingine ikitokea hali kama hii, tunapata mabadiliko chanya ya celli ambayo yanaweza kubadili mwenendo wa jamii ya viumbe husika.

Mionzi yenye uwezo wa ku-’ionize’ inaweza kutoa elektroni kwenye moleculi za DNA. Kitu hiki kikitokea, kinaweza kupelekea celli kufa au kupelekea DNA kukosa uwezo wa kutoa muongozo kwa celli hiyo na hivyo celli huendelea kuishi ila vivyo-sivyo na kupelekea kansa. Na kama uharibifu ukifanyika kwa namna flani inayoruhusu, basi celli hiyo itaweza kujiongeza na hatimaye uvimbe(tumor) utatokea kwenye sehemu ya mwili na hatari zaidi itatokea iwapo celli hiyo ikisambaa sehemu nyingine mwilini.

SOMA PIA  Ushirikiano mzuri kati ya Dropbox na Google Drive

Mionzi na Vifaa vya Kielektroniki:

Redio ya simu yako inatoa mionzi ya nguvu kati ya masafa ya MHz700 – GHz2.5. Wayalesi inafanya kazi kati ya GHz 2.4 – 5. Bluetooth nayo inacheza kwenye masafa ya GHz 2.4 pia. Hata katika nguvu ya juu kabisa ya vifaa vyetu vya kielektroniki vinafanya kazi kwa nguvu ya chini ya 1/1200 ya nguvu ya mwanga na 1/9600 ya nguvu inayohitaji ku-’ionize’ au kuchana elektroni kutoka kwenye atomu ambayo ni terahertz 2400. X-ray inatoa nguvu mara millioni 12 ya nguvu inayotoa simu yako na pia mionzi ya gamma ambayo ina madhara.

Tafiti mbalimbali , Wanasayansi na hata Madaktari Wanakubali kuwa Hakuna Shida:

Kwa mfano, Taasisi ya Saratani ya Marekani (National Cancer Institute at the U.S. National Institutes of Health) inakubaliana ya kwamba “there is no evdence from studies of cells, animals, or humans that radio frequency energy can cause cancer.” Kwa kiswahili, wanasema hakuna ushahidi kutoka tafiti za celli, wanyama au binadamu zinazoonesha masafa ya redio yanaweza kuzua saratani.

The American Cancer Society nao wansema, “the RF waves given off by cell phones don’t have enough energy to damage DNA directly or to heat body tissues”. Yani, mionzi inayotolewa na simu haina nguvu ya kutosha kuharibu DNA moja-kwa-moja au kuunguza kiungo vya mwili. Tafiti ya miaka 20 ya Jarida la Epidemiology *(The Journal of Epidemiology) ya nchi za Scandinavia hazikupata uwiano kati ya matumizi ya simu na saratani. Tafiti ya nchini Denmark ya Swiss Tropical and Public Health Institute ililinganisha uwezekano wa kupata saratani kati ya watumiaji wa simu na wasio watumiaji kutoka mwaka 1990 hadi 2011 na kukuta kwamba hakuna muongezeko wa hatari  ya kupata saratani.

SOMA PIA  Hizi ndio apps salama zaidi kwa kuchati - ripoti ya Amnesty International, 2016!

Cha Msingi:

Kiukweli, kibaya kinachoweza kufanywa na simu yako ni kuongeza kidogo joto la mwili na hata hivyo, hilo joto lote linatoka kwenye vifaa vya kieltroniki na betrii, na sio mionzi.

Kama kawaida, kila kitu kizuri hakiwezi kukosa ubaya. Simu zetu na vifaa-kompyuta vya kisasa vinatuwezesha kushirikiana kwa karibu zaidi na kukamilisha shughuli zetu za kila siku kwa ufanisi zaidi ila, ubaya wake unaonekana hasa kijamii na kitamaduni. Inaweza kukubalika kwamba vifaa hivi vinapunguza jinsi tunavyoshirikiana na watu karibu yetu. Si rahisi kuboreka na kukosa kitu cha kufanya unapokuwa na simu ya mkononi ya kisasa. Haulazimiki kuongea na mtu unapokuwa unasubiria gari kituoni au hata huduma hospitalini. Mazungumzo kati ya binadamu yanapungua na hata uwezo wa kuanza na kuendesha mazungumzo unapungua siku hizi. Pia, pamoja na mambo mengine kama uwezo wa kuandika lugha fasaha, uvumilivu, simu na teknolojia ya mawasilano inabadili tamaduni zetu kutokana na urahisi wa mawazo ya kigeni kuingia kwenye jamii yetu ya kisasa ila katika suala la saratani, simu haziwezi kuhusishwa.

Chanzo: Derek Kessler, ‘Relax, your smartphone and smartwatch won’t — and can’t — give you cancer’, AndroidPolice.com .

ecay

Ninafuatilia teknolojia kila siku na ninapenda kutoa ujuzi wangu kuhusu teknolojia. Karibu tuzungumze kuhusu teknolojia hapa teknokona!

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania