Kwa miaka kadhaa sasa Xiaomi wamekuwa wakileta ushindani wa aina yake kwenye biashara ya simu janja na hii inatokana na rununu zake kupata wateja wengi sehemu nyingi duniani.
Niwe mkweli katika makampuni ambayo yamekuwa yakipata umakini wangu kila wanapotoa bidhaa basi Xiaomi ni miongoni mwao ambao hivi jaribuni wametoa Redmi Note 10s. Hii ni simu ambayo inaendana na nini ambaccho soko la sasa linataka. Fuatanami kupata undani wa rununu husika.
Sifa za Redmi Note 10s
Katika maisha ya sasa matumizi ya simu janja yanaonekana kuwa na umuhimu wake hasa kutokana na ukuaji wa teknolojia. Swali rahisi tuu simu nzuri ina sifa zipi?
Kioo :
- Ukubwa: inchi 6.43 (1080 x 2400px)+kioo chake ni Corning Gorilla Glass 3
- Ubora: AMOLED, ung’avu wa hali ya juu sana+umbo mithili ya tone la maji kwenye kamera ya mbele
Memori :
- Diski uhifadhi: 64GB/128GB+uwezo wa kuweka memori ya ziada
- RAM: 6GB/GB 8
Kamera :
- Kamera Kuu: MP 64, 8, 2 na 2+taa moja ya kuongeza mwangaza sehemu ambazo kuna mwanga hafifu
- Kamera ya Mbele: MP 13
Betri/Chaji :
- Li-Ion 5000 mAh
- USB-C 2.0+uwezo wa kuchaji haraka kwa nguvu ya 33W (50% kwa dakika 25, 100% ndani ya dakika 74)
Kipuri mama :
- MediaTek Helio G95 SoC
Programu Endeshi
- MIUI 12.5, Android 11
Uzito
- Gramu 178.8
Rangi/Bei :
- Nyeupe, Bluu na Kahawia
- GB 6/64-bei bado haijafahamika, GB 6/128-$339 (zaidi ya Tsh. 779,700) na GB 8/128-bei bado haijafahamika bei ya ughaibuni
Redmi Note 10s ina sehemu ya kuchomeka spika za masikoni, teknolojia ya kutumia alama ya kidole, NFS, Bluetooth 5.1.
Hao ndio sio Xiaomi ambao wana simu janja. Kiujumla ni simu janja yenye mengi mazuri na nzuri zaidi kwa wale wanaopenda kucheza magemu. Sasa kazi kwako kuweza kuitafuta na kuimiliki.
Vyanzo: GSMArena, The Indian Express
No Comment! Be the first one.