Moja katika maswali mengi ambayo watu wanajiuliza kutoka katika logo ya Apple ni kwamba kwa nini logo hiyo imeng’atwa upande mmoja?
Moja kati ya sifa kubwa katika kampuni la Apple ni kuwa na ubunifu wa hali ya juu katika bidhaa zake ambao unatofautisha bidhaa za Apple na bidhaa zingine nyingi. Kazi kubwa ya bwana Steve Jobs ilikuwa imejikita sana katika ubunifu wa vifaa ukilinganisha na teknolojia.
Logo hiyo ina tunda la tufaha (Apple) ambalo kwa upande wake wa kulia kuna kipande hakipo (kimeng’atwa), lakini kwa nini logo hiyo iko hivyo?
Mtu ambaye alitumika katika kutengeneza logo ya kampuni hiyo ni Bw. Rob Janoff na sababu kubwa aliyoamua kuifanya logo ya kampuni hiyo kuwa na tufaha (apple) ambalo halina kipande sehemu moja ni kwa kuwa alitaka kulitofautisha tunda hilo na tunda la cheri (cherry)
Hiyo ndio sababu kubwa lakini ngoja tuangalie katika logo zingine za mwanzo jinsi zilivyokuwa kabla yah ii inayotumika sasa
- Logo Ya Kwanza
Logo ya kampuni ya mara kwanza kabisa ilikuwa imetengenezwa spesheli katika kumuenzi gwiji la sayansi Bw. Isaac Newton hasa pale alipogundua uvutano (gravity). Logo hiyo ilimuonyesha Bw. Isaac amekaa chini ya mti ambapo mti huo una tunda la tufaha (Apple) ambalo linawaka. Katika logo hiyo kuna usemi ambao umeandikwa
Newton…A Mind Forever Voyaging Through Strange Seas of Thought…Alone tafsiri ya haraka haraka ni kwamba “Akili inawaza mambo mabali mbali ikiwa anaewaza yuko peke yake”
Japokuwa logo hii ilikuwa ni ya aina yake, lakini ilikuwa na mambo mengi sana na mtu wa tatu kati ya wale wa kwanza kabisa katika kugundua kampuni la Apple, Bw. Ronald Wayne aliliona hilo. Bw. Ronald Wayne baada ya muda aliamua kuuza hisa zake (10%) za kampuni hiyo kwa dola za kimarekani 800 cha ajabu ni kwamba kama anagekuwa na hisa hizo mpaka sasa angekuwa na utajiri zaidi ya dola bilioni 2 za kimarekani
- Logo Ya Pili
Kampuni likaamua kutengeneza logo nyingine ambayo itakuwa ya aina yake na ambayo itaweza kumvutia mtu. Logo hii ilitengenezwa mwaka 1977 na pia ilitengenezwa na Bw. Ronald Janoff ambapo ilikuwa imeongezewa rangi. Kampuni liliamua kuongeza rangi katika logo ya kampuni ili mradi tuu kujiweka karibu na kuvutia macho ya wateja wao. Kitu kingine cha aina yake katika logo hii ni kule kung’atwa kwa upande mmoja wa tunda. Logo hii ilitumika katika bidhaa zote kutoka kampuni la Apple mpaka mwaka 1998.
- Logo Ya Tatu
Kwa kipindi cha mwaka 1998 mpaka mwaka 2007 kampuni la Apple lilizindua logo 3 ambazo zinafanana (hazikuwa na tofauti kubwa ndani yake). Jambo hili linazifanya logo hizi kuonekana kama moja tuu yenye maboresho kidogo
Katika mwaka 1998 logo ya rangi ya blue ilizinduliwa kutokana na kuachiwa kwa kompyuta za iMac. Logo hii ilianza kutumiwa baada ya Steve Jobs kurudi katika kampuni hilo na iliachwa kutumiwa mwaka 2000.
Kutoka mwaka 2000 mpaka 2002 logo ambayo haikuwa narangi ilianza kutumiwa. Logo hii ilikuwa na mantiki kama ya glasi na usilva ndani yake.
Kutoka mwaka 2002 na kuendelea Apple walitumia logo nyingine ambayo iliambatana katika uzinduzi wa Os ya Panther OS. Logo hii iliendelea kutumiwa mpaka mwaka 2007 ambapo ndipo iPhone ya kwanza ilizinduliwa.
- Logo Ya Nne
Kuanzia mwaka 2007 na kuendelea Apple waliamua kuwa na logo nyingine ambayo iko kawaida sana katika muonekano na staili ya kawaida sana. Hii iliipelekea kampuni ya Apple kuwa na logo flani hivi ya kawaida yenye weusi mzuri.
Hiyo ni stori fupi ya kampuni la Apple katika logo yake. Ni kitu kizuri sana walichokifanya kampuni la Apple kwani makampuni mengi huwa wanabadilisha kabisa logo zao pale wanapoona wanahitaji kubadilika katika utendaji na kila kitu. Kampuni la Apple limeweza kuwa na logo moja (japo wamefanya marekebisho madogo madogo) kwa kipindi cha muda mrefu.