Tofauti na watu wengi wakubwa katika ujasiriamali, kama ukimuona Bw. Jack Ma katika mitaa akiwa peke yake kuna hati hati kubwa kuwa huwezi kumtambua
Hata historia yake kwa ujumla ni tofauti sana ukilinganisha na wajasiriamali wengine katika swala zima la teknolojia kama vile Steve Jobs wa kampuni la Apple, Mark Zuckerberg au hata Bill Gates.
Sababu ni kwa sababu hakuwa mtu ambae ana akili nyingi sana akiwa shule na pia hakumaliza katia vyuo vikubwa vya elimu ya juu kama wengine walivyomaliza katika chuo cha Havard. Hata hakuwa maarufu katika miaka yake ya ishirini kama wengine
Jack Ma stori yake ni ya aina yake kwani alikosa kazi za chini kabisa kama vile kupata kazi katika migawaha mikubwa kama KFC.
Stori kama hizi zinaweza kufananishwa na watu wengi sana duniani hasa wale wenye kipato cha chini kabisa. Stori yake haielezei tuu vitu ambavyo alikosa au alishindwa kupata bali inaelezea hata jinsi alivyopambana ili kuhakikisha anapata kile alichokuwa anakitaka na kuviwekea mkazo na hatimaye kuvipata vitu hivyo.
Jack Ma ni mwanzilishi wa mtandao mkubwa ambao unahusisha mauzo ya bidha kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Mtandao wake mkubwa huko uchinani unajulikana kama Alibaba ambao unatengeneza mabilioni ya dola za kimarekani kwa mwaka.
Kama hujui hata jina la Jack sio jina lake halisi ni jina alilopewa na mmoja kati ya watalii ambao kwa kipindi hicho alikuwa anafanya kibarua cha kuwaelekeza sehemu tofauti tofauti za nchi yake. Mmoja kati ya watalii hao alikuwa karibu sana na yeye na jambo hilo likapelekea yeye kumuita Jack kwani jina lake la kichia lilikuwa ni gumu katika mdomo wa mtalii huyo katika kulitamka
Mbali na hapo pia Jack alifeli mara tatu katika mitihani ya chuo lakini alifanikiwa kumaliza akiwa na shahada (degree) ya kiingeeza kama mwalimu.
Jack alianza mtandao wa Alibaba mwaka 1999 akiwa na mkewe pamoja na marafiki zake 17 wengine. Hatimaye walianzisha tovuti (mtandao) na ukawa unajikita sana katika biashara ya kuwaunganisha wauzaji na wanunuaji wa vitu. Mtihani wake mkubwa ulikuja pale mtandao wa Ebay ulipokuja katika soko la china
Jack alipoona ushindani unakuwa mkubwa sana, ili kuipa moyo timu yake aliwaambia ” Ebay is a shark in the ocean. We are a crocodile in the Yangtze river. If we fight in the ocean, we will lose. But if we fight in the river, we will win” Akiwa na maana kuwa “Ebay ni papa katika bahari na wao ni mamba katika mto wa Yangtze. Kama wakipigana katika bahari watashindwa, ila kama wakishindana katika mto wao watashinda”
Hapa akiwa na maana kuwa biashara yao na nguvu zao nyingi waziwekeze katika soko la china aumbalo wanalijua vizuri.
Ukweli wa msemo wake ulikuja kuonekana baada ya mtu timu nzima ya Jack Ma kuweka nguvu nyingi katika soko hilo. Ebay ambao hawakulielewa sana soko la uchina walijikuta wakishindwa kufanya kazi katika soko hilo na kufunga biashara zao katika soko la uchina. Hatimaye mamba akashinda
Uongozi wa Bw. Jack ni wa aina ya utofauti sana kiasi cha kwamba watu wan je ya timu yake walizani kuwa jamaa ana ugunjwa wa akili (au ni chizi tuu). Licha ya hivyo lakini watu wake wa ndani (timu) ndio waliokuwa wakijua dhahiri dhamira yake na maono yake katika biashara hiyo.
Jack Ma alikuwa mstari wa mbele katika kupinga kuanza kazi saa mbili na kumaliza saa kumi na moja jioni kwani alikuwa akijua dhahiri kuwa kampuni lake bado halijapata mafanikio makubwa na ili kuyapata iliwabidi wafanye kazi kwa bidii na wavuke mipaka ya mida ya kufanya kazi ya kawaida.
Jack Ma alikuwa tofauti sana na wajasiriamali wengine. Alifanya mbinu zozote ambazo zilikuwa ndani ya uwezo wake ili kuijenga timu yake katika kuhakikisha inakuwa katika baadhi ya timu bora.
Katika mahojiano ambayo alifanya na moja ya kituo cha habari alikiri kuwa katika kipindi cha mwanzo cha Alibaba hakuwahi kuandika hata ‘Code’ moja katika mtandao huo au hata kufanya mauzo au manunuzi.
Stori hii ya Jack Ma inaelezea kwa kina kuwa sio lazima ufanikiwe kwa kile unachokifanya sasa ili ufanikiwe katika maisha. Unaweza ukafeli kwanza aua hata ukabadilisha kitu unachokifanya kabla ya kuwa mtu ambaye umefanikiwa katika maisha. Mambo ni mengi sana ya kufanya na fursa zinaongezeka kila siku, cha kufanya ni kujipangilia katika mambo yako.