fbpx
apps, instagram, Intaneti, Mtandao, Teknolojia

Instagram yazidi kuiiga Snapchat, yaleta face filters na Hashtags

instagram-yazidi-kuiiga-snapchat-yaleta-face-filters-na-hashtags

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Instagram imeendelea na tabia yake ya kuiga vitu kutoka mtandao wa Snapchat, Instagram leo inaleta maboresho katika mtandao wake ambayo pamoja na yote yataleta vitu vitatu ambavyo vyote vipo na vinafanya vizuri katika mtandao wa Snapchat.

Instagram
Baadhi ya vitu vilivyoongezwa ni Ufutio ama eraser na pia uwezo wa kutumia Hashtag kama stika.

Instagram imeendelea na mchezo wa kuuiga Snapchat baada ya kuleta mabadiliko mapya, sasa kama ilivyokuwa kwa Snapchat watu wataweza kuweka filter katika selfie zao ( kama zile za masikio na ulimi wa mbwa katika Snapchat)  unaweza kuweka Hashtag katika picha ambayo itakuwa kama stika pia watumiaji wanaweza kufuta michoro ambayo wameichora katika picha kwa kutumia kifutio ama eraser.

Je mtindo huu wa kuiga Snapchat unawasaidia Instagram?! ama ndio unauua mtandao huu?.

Ukweli ni kwamba Instagram imesaidiwa saana na kuiga kutoka kwa Snapchat maana Stories ambayo ni kitu kilichoigwa  imefanikiwa kufikia watumiaji milioni miambili ukilinganisha na watumiaji milioni mia moja na sitini ambao walilipotiwa kutumia Snapchat wakati ikijiandikisha katika soko la hisa.

INAYOHUSIANA  'Android' Anaswa Akikojolea Apple ktk Google Maps
Instagram
Baadhi ya filter zilizoletwa ambazo kabla zilikuwa zinapatikana Snapchat pekee.

Mabadiliko haya yanategemea kuwafikia lini watumiaji?

Kwamujibu wa mtandao wa  Techcrunch mabadiliko haya yanaanza kutolewa leo kwa watumiaji wa ulimwengu mzima na wa OS zote, hivyo siku si nyingi tutaanza kuona mabadiliko haya katika akaunti zetu.

Tuambie unaonaje mabadiliko haya na mtindo huu wa Instagram kuiga vitu kutoka Snapchat, Je watatoboa ama ndio wanajimaliza wenyewe??

Endelea kufuatilia Teknokona kwa habari tofauti tofauti za teknolojia kwa wakati

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Nickson