Ni wazi kuwa ndani ya mtandao wa Facebook kuna magemu mengi tuu, kitu ambacho kilipelekea kampuni kuanzisha App, Facebook Gaming kwa ajili ya magemu hayo.
App hii iliachiwa katika masoko yote makubwa ya App kama vile iOS na Android na sio kwamba App ilikua ikifanya vibaya la-ha-sha!

Vyanzo vingi vinasema kuwa pengine Facebook imefikia uamuzi huu wa kuachana na huduma hiyo baada ya kuona huduma ya magemu kwa upande wa mtandao wa kijamii wa Twitch ndio unashikilia namba moja kwa sasa.
Sasa unaweza ukajiuliza wanawezaje kufunga Facebook Gaming moja kwa moja? Jibu ni rahisi tuu hapa kinachofanyika ni kwamba baada ya Facebook Gaming kufungiwa kabisa..
..hivyo watu itabidi kutumia vitu vyao ndani ya magemu hayo mpaka kufikia agosti 28, baada ya hapo taarifa za muhimu tuu zitaweza kuhamishwa kwenda katika mtandoa wa Facebook wa kawaida.

Cha msingi kama ulinunua kitu kupitia katika App hiyo jaribu kukitumia zaidi mpaka kufikia tarehe tajwa angalau uwe huidai chochote App hiyo.
😬 pic.twitter.com/P6mDEFRheo
— Gothalion (@Gothalion) August 29, 2022
Kingine kizuri kuhusiana na App hii ni ule uwezo wake wa kuwafanya wachezaji kushindana kwa kautumia akaunti zao za mitandao ya kijamii ya Facebook….mfano kupitia marafiki zako unaweza kujua ni nani anaeongoza katika gemu fulani
Hili ni jambo la kushangaza kidogo kwani kampuni mara kwa mara imekua ikisema kuwa inajikita pia katika teknolojia ya magemu sasa cha kushangaza wanafunga jukwaa hili.

Pengine labda kuna plani kubwa zaidi sio? Pengine labda miradi yake ya VR ambayo inatarajiwa kuja/kutambulishwa hivi karibuni itakua na huduma za magemu za kutosha.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je ni magemu gani ushawahi kucheza katika mtandao wa Facebook? Je ushawahi kutumia App ya Facebook Gaming?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.