Twitter ni moja kati ya mitandao ya kijamii ambayo ni maarufu sana, mara kwa mara imekua ikija na maboresho kadha wa kadha na hata kuongeza vipengele vipya na sasa wanakuja na Co-Tweet.
Kwa sasa mtandao huo wa kijamii unakuja na huduma ya Co-Tweet. Hebu pata picha watumaji wawili wa mtandao huo wakishirikia katika kuhakikisha kuwa wanatuma Tweet moja.

Kipengele hichi lakini kwa ssasa ni kwamba kipo kwa watu wachachee tuu ambao kwa sasa wamekua kama sehemu ya majaribio kwa kipengele hicho.
Ni kawaida sana kwa mitandao ya kijamii kwa sasa kuchagua baadhi ya watu kuwa kama sehemu ya kujaribu kipengele kipya kabla ya kukiachia kwa watu wote.

Sasa basi ufanyaji kazi wa kippo hivi……
Hapa kinachofanyika ni kwamba muandishi wa kwanza ataandika Tweet kama kawaida na kisha kumualika mwandishi mwingine (Wa pili) na hapa atakua na uwezo wa kum’tag kama muandishi mwenza.
Share a Tweet, share the cred.
Now testing CoTweets, a new way to Tweet together. pic.twitter.com/q0gHSCXnhv
— Twitter Create (@TwitterCreate) July 7, 2022
Lakini pia ili mambo yaende hivi inabidi huyo muandishi wa pili akubali sababu kwake yatakuja kama maombi katika ushirika huo.
Vyanzo mbali mbali pia vinahisi katika swala zima la majibu ya tweet husika ni lazima yataenda moja kwa moja kwa mtu wa kwanza kabisa (mmiliki halali) wa tweet hiyo.
Kwa kifupi majibu hayawezi kwenda kwa wote labda wote wawe wametajwa katika Tweet hiyo ya majibu lakini hivi hivi haiwezekani.
This is a CoTweet from me and Emma
— Kelly Vaughn (@kvlly) July 7, 2022
Kama kipengele hichi kitajizolea umaarufu mkubwa basi hakina budi kuachiwa duniani kote ili watu wakifurahie Zaidi.
Chanzo: The Verge
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je kipengele hichi umekipokeaje?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.