fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Mtandao Mtandao wa Kijamii Snapchat

SnapChat: Watumiaji Wa Uk Wanaweza Kwenda Jela Kwa Kunakili Snap!

SnapChat: Watumiaji Wa Uk Wanaweza Kwenda Jela Kwa Kunakili Snap!

Spread the love

Utumiaji wa mtandao huu wa kijamii inabidi kuwa wa umakini sana kwani kuna sheria nyingi na sera ambazo zinauongoza. SnapChat ina misingi nakanunu kadha wa kadha kama mitandao mingine ya kijamii ila kama kawaida yetu tunapenda kuanza kutumia mitandao hii bila kusoma kanuni zake.

Ukiwa ndani ya mtandao wa SnapChat inakubidi kuwa na umakini pindi unapoamua kuchukua ‘Screenshot’ juu ya jambo Fulani ambalo mtu ameliweka katika akaunti yake. Kitu cha ina yake katika mtandao huu ni kwamba kama umechukua nakala ya kile alichokituma (screenshot) basi mtumiaji atapewa taarifa mara moja na mtandao huu kama umefanya hivyo.

Kumbuka unaweza ukachukua nakala ya kitu ambacho mtu amekiweka katika mtandao wake wa SnapChat na ukaamua kukisambaza kwa watu bila idhini yake. Ukifanya hivyo utakuwa umemkosea sio? Na hasa kama hataki au hapendi kile kitu kionekane nje ya SnapChat.

SnapChat

SnapChat

Ukiwa UK kama umechukua nakala ya kitu alichokituma katika SnapChat bila idhini yake na mbaya zaidi ukaamua kukisambaz akwa watu basi mtu anaweza akaamua kukushtaki katika vyombo vya sheria.

Akishinda kesi hukumu itafutwa. Hii ni kwa sababu vitu ambavyo watu wanavituma katika mtandao huo wa SnapChat vinalindwa na sheria

Sheria hii inasema kuwa “itakua nje ya sheria kwa mtumiaji wa SnapChat kunakili picha na kuifanya ipatikane katika jamii bila ya kupata kibali toka kwa mwenye picha hiyo”

SOMA PIA  TikTok yaendelea kupingwa Marekani, Afisa wa juu wa taasisi ya Mawasiliano ataka iondolewe

Katika sera ya usiri ya Snapchat inasemma kuwa mara nyingi meseji zinakuwa zinafutwa katika hifadhi zao (server) endapo kampuni inabaini kuwa meseji hiyo imesomwa au imepita muda wake (expire). Japokuwa jambo hili sio kila saa linawezekana kwa mfano katika kujibu meseji mtu unaweza ukaamua kusevu meseji ili kukupa mwangaza juu ya kitu mnachokiongelea mbeleni (watumiaji wa SnapChat watanielewa zaidi)

Kwa kuwa picha na video zinapotea ndani ya kipindi cha muda mchache basi watumiji wengi wanfurahia kutumia mtandao wa SnapChat katika kutuma na kupokea picha ambazo hazina maadili (mara nyingi)

Mfano Wa Snap Katika SnapChat

Mfano Wa Snap Katika SnapChat

Lakini hata hivyo watumiaji wanaweza kuchukua nakala (screenshots) za picha hizo, na ikitokea hivyo sera ya kampuni inasema kuwa itakuwa inawatumia wenye akaunti taarifa kama kuna mtu amechukua nakala juu kitu walichokiituma.

SOMA PIA  Facebook kujiweka pembeni na vitu vyenye maudhui ya kutia shaka

Hapo unaweza ukashangaa unaanza kutwangwa maswali kama, Kwa nini umechukua picha yangu bila kibali change? Kutoka kwa mwenye picha.

Sheria kali kama hii ikija na sehemu kama Tanzania sijui itakuaje? Pengine watu watakuwa wantuma picha ambazo hazina maadili zaidi kwakujua kama wakienda kushtaki kwa serikali watalipwa fidia n.k.

Niandikie mawazo yako sehemu ya comment hapo chini kuhusiana na jambo hili. Tembelea TeknoKona kila siku kwakupata habari moto moto za teknolojia. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania