Microsoft iko katika maandalizi ya kuandaa Windows 10 ambayo ipo spesheli kwa ajili ya serikali ya china. Jambo hili linakuja baada ya serikali hiyo kuomba jambo hili.
China imeona kuwa windows za kawaida zenye majina ya Windows 10 home, Windows 10 Pro, Windows 10 Mobile na Windows 10 Enterprise zilikuwa hazijitoshelezi kikamilifu kwa matumizi ya serikali ya china.
Jambo hili ndilo lililopelekea serikali ya china itoe ombi kwa kampuni la Microsoft ili ishirikane na shirika la china katika kuhakikisha wanapata toleo jingine la Windows 10 ambalo litakuwa spesheli kwa ajili yao.
Kutokana na ushirikiano huo jina la Wondows litaitwa: Windows 10 Zhuangongban. Mkurugenzi mkuu wa Microsoft huko china, Bw. Ralph Haupter ameiambia Caixin (Gazeti la china) kwamba Windows 10 Zhuangongban inaweza kuendesha ‘software’ zote ambazo zinakubalika katika Windows lakini hakusema zaidi kuhusiana na Windows hiyo spesheli kwa ajili ya china kama vile mabadiliko na vitu vitakavyo ongezeka.
Kumbuka hii sio Os pekee ambayo serikali ya china imekua na mpango nayo. Waliwekeza katika OS ambayo inajulikana kama NeoKylin ambayo ilikuwa ni ya Linux ambayo ilikuzwa na china. Os hiyo imekuwa ikitumika katika sehemu kubwa tuu kwa kipindi cha miaka kadhaa.
Ukilinganisha Windows 10 Zhuangongban na ile ya linux ni kwamba Os ya Microsoft ina uwezo mkubwa kwani ina uwezo wa kuingiza ‘software’ nyingi tuu. Ukiangalia kwa ‘software’ ambazo zinakuja na Windows 10 Zhuangongban kama vile Office 365 unaona kabisa ni rahisi kabisa kwa Windows hiyo kupendekezwa na kutumiwa zaidi na zaidi.
Kuna baadhi ya wataalamu wa teknolojia wamependa ukaribu wa Microsoft na serikali ya china. Hii ni kwa sababu serikali inaweza ikaiambia Microsoft ifanye vile inavyotaka yenyewe bila ya kuangalia sera za watuamiaji wake