fbpx

Microsoft kuachisha Programu ya Paint katika Windows 10

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Kuna uwezekano mkubwa Microsoft kuondoa programu ya Paint katika sasisho (update) jipya la Windows 10.

Programu ya Paint inayomuwezesha mtumiaji kuweza kutengeneza michoro mbalimbali kwa urahisi na bila ujuzi mkubwa sana wa kisanii imekuwa katika matoleo ya programu endeshaji ya Windows tokea Novemba mwaka 1985 kwenye toleo la Windows 1.0.

Muonekano ndani ya programu ya Paint

Muonekano ndani wa Paint

Programu ya Paint imekuwa ni rahisi kwa watumiaji wengi katika suala la ubunifu wa picha ukilinganisha na programu zingine zinazoitaji ujuzi zaidi kama vile Adobe Photoshop.

INAYOHUSIANA  Sasa unaweza kutumia Instagram bila ya App yao rasmi

Imekuwa ikipata maboresho mapya mara kwa mara na wakati wote imeendelea kuwa programu ya bure. Katika sasisho (update) jipya linalokuja lililopewa jina la Windows 10 Fall Creators Update programu hiyo imewekwa kwenye kundi la vitu vinavyouliwa.

Tayari Microsoft wameshaleta programu mpya ambayo ni maboresho zaidi ukilinganisha na hii ya Paint, wameipa jina la Paint 3D na inapatikana kwenye soko la apps katika Windows 10.

programu ya paint windows 10

Muonekano wa Paint 3D – Inapatikana katika soko la apps ndani ya Windows 10.

Wengi wanaamini kuna uwezekano mkubwa katika sasisho hilo Paint 3D ikachakua nafasi ya programu ya Paint.

INAYOHUSIANA  Twitter: Watu wanatwiti zaidi, ila twiti zao si ndefu sana

Je umeshatumia programu hii? Tuambie mtazamo wako juu ya uamuzi huu wa Microsoft.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.