fbpx
apps, Kompyuta, Windows

MiniLyrics: Programu nzuri ya kuonesha lyrics za nyimbo kwenye kompyuta yako

minilyrics-programu-ya-kuonesha-lyrics-za-nyimbo-kwenye-kompyuta
Sambaza

MiniLyrics ni moja ya programu muhimu kuwa nayo kwenye kompyuta yako kwa watu wanaopenda muziki na wanaopenda kuimba kupitia usomaji wa maandishi ya nyimbo – lyrics.

MiniLyrics ni programu ya bure kabisa, na ni programu iliyokuwepo kwa miaka kadhaa sasa. Ninachoipendea ni kwamba haina mambo mengi na inafanya kila inachotakiwa kukifanya tena bila longolongo.

minilyrics lyrics za nyimbo kwenye kompyuta
MiniLyrics: Pata mashairi / Lyrics za nyimbo kwenye kompyuta

Machache kuhusu programu hii:

  • Programu hii inafanya kazi moja kwa moja kwa kuzitambua nyimbo zinazocheza kwenye kompyuta yako kupitia programu za iTunes, Windows Media Player, Winamp n.k.
  • Utaweza kuona lyrics za nyimbo hizo huku ukipata nafasi ya kuendelea kufanya kazi zako zingine kwneye kompyuta yako.
  • Programu inauwezo wa kutafuta na kudownload lyrics za nyimbo moja kwa moja mtandaoni bila uhitaji wako wa kufanya chochote – hakikisha tuu kompyuta ina intaneti
  • Lyrics zikishadownloadiwa zinahifadhiwa kwenye kompyuta yako, hivyo muda ujao hauhitaji kuwa na intaneti ili ziweze kufanya kazi
INAYOHUSIANA  App Bora Kwa Ajili Ya Kamera Za iOs Na Android!

Programu inakuja pia na uwezo wa kuonesha lyrics bila kuzuia kipanya chako kubofya vitu vya chini yake. Yaani lyrics zinaweza tokea juu ya programu nyingine unayoitumia.

Haya ndio machache kuhusu programu hii ya MiniLyrics. Programu hii inapatikana kwa ajili ya kompyuta za Windows na Mac.

Kodownload, tembelea tovuti – MiniLyrics

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |