Mtandao wa Instagram umetangaza kwamba utaongeza urefu wa video ambazo watumiaji wake wanaweza kutupia katika akaunti zao, sasa watumiaji wa Instagram wataweza kuweka video za hadi sekunde 60 badala ya ile ya sekunde 15 ambayo ndiyo ipo mpaka sasa.
Katika post waliyoiweka Instagram katika tovuti yao wanasema kwamba wanataka kuleta namna mpya yakuburudisha katika kutengeneza na kuangalia video katika mtandao huu, pia wakaongeza kwamba hii moja tu ya mambo ambayo wanategemea kuyaanziasha mwaka huu.
Imesemekana kwamba kumekuwa na ongezeko la asilimia 40 la muda uliotumika kuangalia video katika mtandao huu kwa miezi 6 iliyopita. Hii inamaana kwamba watumiaji wa Instagram wanaoangalia video wanazidi kuongezeka na pengine ndio maana mtandao huu unataka kutumia hii nafasi.
Pamoja nakuongeza urefu wa video Instagram pia watumiaji wa vifaa vya iOS kama vile iPhone na iPads watapata uwezo wa kutengeneza video kutoka katika clip za kwenye camera roll, huduma hiii itaenda katika soko la iOS wiki hii.
Mabadiliko haya yameanza kuonekana jana lakini yataendelea na baada ya mwezi mmoja watumiaji wengi watakuwa wameyapata. Ingawa wenye akaunti za matangazo walipata huu uwezo miezi miwili kabla hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa watumiaji wa kawaida.
Baadhi ya tafiti zinaonesha kwamba video fupi ambazo hazizidi muda wa dakika moja zinakuwa na watazamaji wengi na watazamaji wanaweza kucheza video mpaka zikafika mwisho ikiwa video husika ni fupi.