Zipo kila dalili za kwamba kampuni kubwa ya Google inaweza kuleta bidhaa ambayo itapambana ama italeta upinzani kwa bidhaa ya Amazon ya Automation ya Echo, taarifa zilizovuja zinadai kwamba Google wanaanza fanyia utafiti kifaa hiki na haijajulikana kama ni lini hasa kitakuwa tayari.
Automation ni sekta ndani ya electronics ambayo inawekea mkazo katika kuhakikisha mitambo na vifaa mbalimbali vinafanya kazi bila ya kumuhusisha binadamu moja kwa moja, mfano ukiingia nyumbani kwako basi taa, feni na TV zijiwashe.
Mpaka sasa katika sekta hii ya Automation ni Amazon pekee ndio wameteka soko hasa kwa bidhaa yao ya Echo ambayo ni spika ya wireless ambayo inaweza kuwa controlled kwa maneno ya mdomo yaani unaweza kuiambia icheze wimbo fulani na ikacheza pia unaweza kuiambia iweke alarm na ikaweka zaidi unaweza kuiambia iwashe vifaa janja ulivyo navyo kama taa feni ama heater.
Miaka miwili iliyopita Google ilinunua kampuni ambayo inajihusisha na utengenezaji wa vifaa janja ya NEST kwa Dola za kimarekani bilioni 2.3, kampuni hii hata hivyo haikufanikiwa kuiingizia pesa Google baada ya kutengeneza vifaa ambavyo vilikuwa na matatizo ya kiufundi. inaripotiwa kwamba NEST hawatashughurika kabisa na mpango huu mpya wa Google kutengeneza bidhaa hiyo mpya pengine ni kwasababu NEST tayari wamejichafua kwa kutengeneza bidhaa mbovu hivyo Gooogle wasingependa kuchafuka.
Google wanahitaji kuingia katika biashara ya Automation kwa sababu wanazo tayari huduma zote ambazo automation inahitaji, Google wanayo huduma ya Google now kwa mfano hii inamaana kwamba wakitengeneza kifaa hicho kitatumia Google now kupokea command kutoka kwa mteja ama kwa kutumia huduma ya Chromecast kwaajiri ya kucheza video unazozipenda.
Eneo la automation bado halijafanyiwa uwekezaji wa kutosha na wataalamu wa mambo wanasema kwamba hili eneo la teknolojia litapiganiwa siku za hivi karibuni na makampuni makubwa kama Apple na Google
Nchi zetu za Afrika mashariki bado zipo nyuma katika teknolojia hasa hii ya Home automation, natoa wito kwa wale wote wapenda teknolojia kuangalia upya matumizi ya teknolojia hii hasa katika majumba na maofisi.
Mfano unaweza kuunga taa zako ndani ya nyumba kuwaka pindi tu kuna mtu ndani ya chumba ama kiyoyozi unaweza kukiweka kifanye kazi pale tu kuna mtu ndani ya nyumba, hii itakusaidia pamoja na mambo yote kupunguza gharama za umeme.