Huko Uholanzi wamekuja na barabara ya kwanza ambayo imetumia teknolojia itakayoiwezesha kufua nguvu za umeme jua, yaani maarufu kama ‘Solar’. Barabara hiyo iliyozinduliwa wiki hii ndiyo ya kwanza duniani na ni ya pembeni kwa ajili ya waenda miguu na waendesha baisikeli. Kwa kuanzia barabara ya sola hii ina urefu wa mita 70.
Teknolojia ya barabara zitakazoweza kufua umeme wa jua imekuwa inaongelewa na tayari watafiti mbalimbali wamejikita katika kuja na njia bora zaidi ya kufanikisha jambo hili. Mafanikio ya barabara hii yatasaidia zaidi katika kujifunza ubora wake na matatizo yeyote yatakayojitokeza katika kukuza teknolojia hii.
Je wametengenezaje?
Seli spesheli za sola zimewekwa ndani ya vioo vigumu ambavyo vimeingizwa na kuzungukwa na zege kali kwa ajili ya kuweka ubora dhidi ya uharibifu. Hivyo watu watakuwa wanatembea juu ya vioo, na hivyo miale ya jua itaweza kufikia seli za sola kwa urahisi.
Matumizi?
Inategemewa teknolojia hii itaraisisha vyanzo vya umeme kwa taa za barabarani na majengo yaliyokaribu. Kutukana na kulazwa na si kuwekwa kiupande inategemewa uwezo wa seli kufua umeme utakuwa asilimia 30 pungufu ukilinganisha na za kuwekwa kiupande hasa kwenye majengo.
Watafiti na serikali ya nchi hiyo imesema watajifunza maendeleo ya barabara hiyo katika miaka mitatu na kufanya maamuzi ya kujenga barabara kama hizo sehemu zingine za miji ya nchi hiyo. Tayari nchini Marekani pia teknolojia hii inafuatiliwa kwa ukaribu zaidi.
Kwetu jua kaliiiiiiiii fikilia kama teknolojia ya barabara za sola ikija Bongo….
| Soma kuhusu Viti visivyo na Miguu – HAPA |
No Comment! Be the first one.