Rununu ni moja ya kitu ambacho kinatuwezesha kufanya mawasiliano kwa haraka na hata kurahisisha shughuli mbalimbali lakini kutokana na ukuaji wa teknolojia kufahamu iwapo simu zako zinafuatiliwa ni jambo muhimu sana.
Katika dunia ya leo watu wanapenda kujua vitu vingi kwenye teknolojia kiasi kwamba mtu anaweza kujikuta anatokea kujihusisha kwa namna moja au nyingine kwenye ulingo huo.
Mbali na hapo kutokana na sababu mbalimbali mtu mwingine anaweza akatumia mbinu fulani fulani kutaka kufahamu mambo yanayoendelea kwenye simu ya mtu mwingine na iwapo utakuwa na mashaka/kutaka kujua iwapo kuna mtu anafuatilia mawasiliano yako ni muhimu kuwa hatua moja mbele zaidi yake.
Jinsi ya kujua kama mtu anafuatilia mazungumzo yako kwenye simu.
i kitu rahisi sana na inakubali kwenye simu janja au hata zile za “Kawaida”. Piga *#61# angalia kama italta majibu “FORWARDED“ basi ujue kuna mtu anafuatilia mazungumzo/ujumbe mfupi wa maneni. Na iwapo itaonyesha neno “NOT FORWARDED” basi uko salama.
Kuondoa au kumzuia mtu asiendelee kutumia namba yako piga ##21# ili kuondoa mazungumzo yako kuchunguliwa kwenye namba yako.
Mfano wa majibu kuweza kujua kama simu yako kuna mtu anafuatilia mazungumzo au la!.
Hivyo ndivyo unaweza kuwa hatua moja mbele (iwapo simu zako zinafuatiliwa) kwa yule ambae anapenda kujua kinachoendelea kwenye simu yako. Wafamishe na wengine ili nao waweze kufahamu.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|