fbpx

Terabyte sio mwisho kwa ukubwa wa memori

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Matumizi ya bidhaa ya kidijiti vyenye uwezo wa kutunza kumbukumbu vinasaidia kweli kweli na katika dunia ya leo ukubwa/udogo wa kifaa (kwa umbo) hauna nafasi kuweza kubashiri ukubwa wa memori.

Suala zima la uwezo wa diski uhifadhi kwa maana ya kwamba ukubwa wake ni jambo ambalo kwa namna moja au nyingine linahusiana namba zake kuwa kwenye kundi la namba shufwa lakini nikuliza ni ukubwa gani unafuata baada ya “Terabyte (TB)” au kama ndio mwisho kwa ukubwa ni watu wachache wataweza kutoa jibu sahihi.

Ukweli ni kwamba Terabyte sio mwisho wa mgawanyiko wa makundi ya ukubwa wa memori; TB inafuata baada ya Gigabyte na rununu nyingi ukubwa wa memori ya ndani yenye GB kadhaa.

ukubwa wa memori

Makundi mbalimbali ya ukubwa wa memori.

Undani wa makundi ya ukubwa/udogo wa diski uhifadhi.

Watu wengi huwa wanapata shida kuweza kutoa mtiririko sahihi kuhusiana na ukubwa wa memori hasa kwa upande wa tarakimu mathalani wengi wetu tutasema 1GB=1000MB kumbe hilo sio sahihi kwa chochote kinachohusisha kompyuta lakini pia teknolojia kwa upana wake.

INAYOHUSIANA  Australia kutumia $ bilioni 50 kununua nyambizi

Sasa basi ni vyema ukafahamu kuwa kompyuta au kifaa kingine ambacho kina uwezo wa kuhifadhi memori ukishatoka kwenye kundi la “Bytes” (ukubwa mdogo kabisa kwenye mgawanyiko wa memori) ambapo byte 1=8 bits basi nyingine zote ili kupata namba nzima tunaanzia 1024 na sio 1000. Mtiriko mzima ni kama ifuatavyo:-

 1 Bit = Binary Digit (0/1)
· 8 Bits = 1 Byte
· 1024 Bytes = 1 Kilobyte
· 1024 Kilobytes = 1 Megabyte
· 1024 Megabytes = 1 Gigabyte
· 1024 Gigabytes = 1 Terabyte
· 1024 Terabytes = 1 Petabyte
· 1024 Petabytes = 1 Exabyte
· 1024 Exabytes = 1 Zettabyte
· 1024 Zettabytes = 1 Yottabyte
· 1024 Yottabytes = 1 Brontobyte
· 1024 Brontobytes = 1 Geopbyte

INAYOHUSIANA  MasterCard Kutambua Malipo Kwa Kutumia Sura za Wateja

Kwa mtiririko huo hapo juu unaweza ukajua kifaa unachokitumia kipo kwenye kundi gani na kama ukitaka kwenda mbele itakayofuata ni ipi. Baada ya kufahamu usisite kushirikisha na wengine au hata kutupa maoni yako.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.