fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Afrika TEHAMA Teknolojia

COSTECH Ndani ya NaneNane: Kilimo na teknolojia!

COSTECH Ndani ya NaneNane: Kilimo na teknolojia!

Spread the love

Ushawahi kuisikia kuhusu COSTECH? Pengine hujawahi. Hii ni tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania ambayo uwepo wake hapa nchini ni kuiwezesha nchi katika  utafiti, ukuwaji na utumikaji wa sayansi na teknilojia na pia kuishauri serikali kuhusu mambo hayo. Hii inamaanisha kwamba, kama una jambo lolote la kibiashara au kisomi linalohusu sayansi na teknolojia na unataka kuifanya kwa makini, basi pale ndio sehemu ya kwanza ya kuanzia.

SOMA PIA  Betri kubwa duniani yazinduliwa; Musk atimiza ahadi yake

Tume hii imekuwa  ikisukuma ukuwaji wa ujuzi katika teknolojia ya kilimo hapa nchini. Katika msimu huu wa Nane Nane, COSTECH imeandika kwenye ukurasa wao kwamba itauonyesha umma harakati hizo katika maonyesho ya Nane Nane yanaoendelea huko lindi na kufika tamati kesho 8/8/2014. Maonyesho hayo yanalenga kukutanisha wakulima na wadau wa kilimo ili kubadilishana mawazo na kuendeleza biashara.

Zaidi, ukurasa huo unamnukuu Dr. Joseph Maziko, mtafiti wa COSTECH akisema kwamba tume hiyo imefadhili miradi 56 katika mwaka 2012 amabayo ina uwezo wa kufanya mapinduzi katika kilimo na kuleta maendeleo ya jamii. Anaendelea kusema, “Tunataka wakulima watumie teknolojia kuongeza kipato chao na kuhakikisha usalama wa chakula hapa nchini.’ Katika Monyesho hayo, tafiti nne zilizofadhiliwa na COSTECH zilionyeshwa. Miradi hiyo ni miradi ya kudhibiti ‘tsetse fly’, ‘fruit flies’ na panya na pia mradi wa kufuga kuku wa kienyeji.” Kama wewe ni mjanja na na upo kwenye kilimo, basi ni vyema kukamata fursa hii na kusogea pale Lindi au kujifunza zaidi kuhusu COSTECH na miradi ya kilimo cha sayansi na kiteknolojia kuptia kwenye mtandao wao

ecay

Ninafuatilia teknolojia kila siku na ninapenda kutoa ujuzi wangu kuhusu teknolojia. Karibu tuzungumze kuhusu teknolojia hapa teknokona!

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania