Ooohh kabla sijaenda mbali, si muhimu kwa wanadada peke yao, bali hata kwa wakaka pia walio na wapenzi wao. Kuna siku siku rafiki yangu mmoja aliniambia kuna app ya kila kitu, ata sikubishana naye. Mdada hakikisha ‘bae’ ana hii app iliasikusumbue siku usizotaka msongo wa mawazo 🙂 . Leo ifahamu P Tracker!
Teknolojia inazidi kutumika kuraisisha maisha yetu ya kila siku katika mfumo wa Apps, P Tracker, kwa kirefu Period Tracker ni app inayowasaidia wadada kutambua mambo yote muhimu yahusuyo mzunguko wao wa hedhi ikiwa ni pamoja na mambo mbalimbali yahusuyo mzunguko huo.
 Kwa kifupi;
- Inatabiri siku ambazo muhusika anaweza akapapa ujauzito kama akijihusisha na ngono
- Inaonesha siku ambazo muhusika ategemee kuanza kwa mzunguko wake tena (Pale mtumiaji atakapotumia kwa mara ya kwanza ataweza kuchagua kama mzungo wake ni wa siku ngapi, hii inawezwa badilishwa ata baadae pale inapobidi)
- Pia inakuwezesha kurekodi hali (mood) yako ya siku mbalimbali, ikitambua ‘mood’ hizi huwa zinaathiri mzunguko.
Katika kumsaidia muhusika kuwa tayari kwa mzunguko mwingine App hii inaruhusu mtu kufanya rekodi za dalili anazokuwa anazipata, app yenyewe tayari inaorodha ya dalili nyingi maarufu tayari. Na kila unavyoitumia ndiyo itazidi kuwa sahihi zaidi katika kutabiri mizunguko ijayo (inatumia historia ya mizunguko yako iliyopita kutabiri ijayo). Kupitia App hii utaweza kuwa na rekodi ya mizunguko iliyopita na ijayo. Kuweza kuona kwa uraisi rekodi za hisia /’mood’ zako. Na mwisho kabisa kuweza kutambua ni siku zipi utegemee nini kama ukijihusisha na ngono.
Ingawa App inaitwa Period Tracker ukishaishusha kwenye simu yako itakuwa inatumia jina la P Tracker.
Je App hii ni nzuri kwa wote wawili? Wewe na mpenzi wako…au ni muhimu kwa wanawake pekee?
Kushusha kwenye simu/tableti yako bofya kulingana na aina yake-> Android, iOS/Apple, Windows Phone
Kusoma kuhusu ‘App ya Wiki’ ya wiki iliyopita bofya ->Â App ya Wiki: Brick Game, Inakukumbusha Enzi Zile
No Comment! Be the first one.