fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Android Apple apps iOS Operating System Samsung simu Teknolojia

App Bora Kwa Ajili Ya Kamera Za iOs Na Android!

App Bora Kwa Ajili Ya Kamera Za iOs Na Android!

Spread the love

Kamera za simu zinatumika sana kuliko kamera za kawaida. Simu-janja zingine ni kamera za kidigitali  kabisa kwa sababu zina MP (mega pixel) kubwa.  Hata hivyo kwa kutumia simu-janja yangu ni rahishi kupiga na  ku ‘share’ katika mitandao tofauti tofati ya kijamii ikiwepo ule maarufu kwa shughuli hizo yaani ‘Instagram’.

Je wewe unapenda kupiga na ku ‘post’ picha nzuri?  VIzuri, siku hizi kuna apps mbalimbali ambazo zina kuwezesha kurekebisha au kuongeza mbwembwe  (edit) picha zako na zikaonekana nzuri zaidi.

Ukiwa na hilo akilini sasa, kuna apps ambazo zinaweza fanya mambo yote hayo, lakini ni zipi?. Kuna Apps nyingi sansa katika simu za Andriod na iOs. Teknokona itakuambia zile nzuri kabisa leo

App Bora Kwa Kuhariri (Edit) Picha Katika iOsAfterlight

Afterlight

Afterlight ni moja kati ya zile App zenye uwezo mkubwa katika ulimwengu wa app za ku ‘edit’ picha. App hii ina aina 15 mbali mbali za vyombo vya marekebisho (adjustment tools).aina 66 za maandishi, filter za picha 59 tofauti tofauti pia inakuwezesha kutengeneza filter zako mwenyewe. ukiachana na yote ina ushirikiano na instagram hivyo kukimaliza tuu ku ;edit; unarusha picha yako moja kwa moja instagram. App hii inapatika kwa dola za kimarekani 0.99 katika AppStore.

SOMA PIA  Facebook Lite : App ya Facebook Isiyokula Data Sana

App Bora Kwa Kuhariri (Edit) Picha Katika AndroidPixlr

pixl

Pixlr ni App Rahisi kutumia, imetengenezwa na Autodesk, kampuni linalojulikana zaidi kwa uinjinia wa ‘software” . kuna machanganyo zaidi ya milioni 200 ya mipaka, rangi na ”effects’ katika App hii.

App Bora Kwa ‘KuShare” (Android na iOs):  Instagram

Instagram

App na pia mtandao wa kijamii namba moja duniani kwa ku ‘share’ picha kwa marafiki na familia. instagram unaarufu wake wa haraka unavuti. Pia ni siku chache tuu zimepita Instagram imepita twitter kwa kutumiwa zaidi dunia. kwa sasa ina watumiaji wa kudumu milioni 300

SOMA PIA: Instagram yaipita Twitter Kwa Ukubwa: Mabadiliko Yanakuja!

SOMA PIA  Karma: Falme za Kiarabu ilidukua simu za iPhones nyingi za wapinzani wake! #Skendo

App Bora Kwa Kuhifadhi Picha (Android na iOs)Flickr

Flickr

Flickr inakupatika 1TB kama nafasi ya kuhifadhi picha zako na hii ni kali kuliko ile App ya Dropbox ambayo inakupa 2Gb tuu za kuhifadhia picha. Kwa kutumia Flickr, utachoka wewe tuu kama unatafuta app ambayo itaishinda flickr kwa nafasi ya kuhifadhi picha zako hautaipata na pia App ni ya kijanja

App Maalum Kwa Ajili Ya iOsTiltShiftGen2

TiltShiftGen2

Unaweza usijue maana lakini ukawa unajua jinsi App hii ilivyo. Jinsi ya kuzifanya picha ziwe kama app hii inavyofanya ni vigumu kidogo maana inahitaji lenzi ambazo ni ngali kwa kamera yako. lakini kwa kutumia hii App kila kitu kitakaa sawa bila ya kutumia pesa nyingi

Jinsi App Ya TiltShiftGen 2 Inavyofanya Kazi

Jinsi App Ya TiltShiftGen 2 Inavyofanya Kazi

App Maalum Kwa Ajili Ya AndroidFacetune

Facetune

Facetune ni App ya ku ‘edit’ picha ipo maridadi zaidi kwa picha za uso na ‘selfies’. ina zana mbalimbali kutoka kwenye kuyafanya meno yawe meupe zaidi, kuondoa chunusi na madoa usoni, kurekebisha rangi na mengine mengi (kwenye picha lakini, Ha!). inauzwa dola za kimarekeni 2.99 bei hii inaonekana ina mwinuko mkubwa lakini kama wewe ni mpenzi wa App nzuri za picha hii ina thamani ya hiyo pesa kiukweli

SOMA PIA  Tweet ya Lukas Podolski wa Arsenal yalipua Bomu Twitter

App Bora Ya HDR Kwa iOsPro HDR X

Pro-HDR-X

Simu-janja ni rahisi kubebeka kulikko kamera zingine, lakini sehemu moja ambapo watu wengi wanachemka ni pale kwenye kupiga picha yenye mwangaza na giza katika picha moja. Kwa ujanja unaweza kutumia App kama Pro HDR X ambayo inapiga picha mbili -yenye mwangaza na yenye ugiza giza- kwa wakati mmoja na kuziunganisha kuwa kitu kimoja ili kuleta HDR (high dynamic range). watumiaji wa Android bado wanaweza kutumia Pro HDR

Kama ni Mpenzi wa Simu-janja za Android na iOs nina imani makala hii imekusisimua na kukufahamisha mautundu mbali mbali yanayohusu picha katika simu yako. Tembeleza kurasa zatu za Twitter, Facebook na Instagram . comment yako ni muhimu sana

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania