Soko la Apps la Apple lina App milioni 1.3 na ina zaidi ya mapakuo (downloads) bilioni 85 tangia kuanzishwa kwa App Store mwaka 2010. Soko la App Store ni la pili kwa ukubwa kufuatiwa na lile namba moja (Google Play Store). Licha ya Hivyo, Apps nyingi zikiwa zinatoka zianzia katika soko la App Store kisha maeneo (masoko) mengine mfano Gemu la Temple run hata na Gemu la Candycrush na mengineyo.
Kampuni ya Apple imetoa orodha ya Apps zilizofanya vizuri zaidi kwa mwaka 2014 na Teknokona tunayo listi ya hizo App hapa.
Na.01. Facebook Messenger; Miezi kadhaa iliyopita Facebook iliwaambia watumiaji kuwa inabidi wadownload App nyingine (Facebook Messenger) tofauti na App ya Facebook yenyewe, Watumiaji wengi walikasirika kwa taarifa hiyo kwa sababu iliwalazimu kuwa na Apps mbili. Baada ya mda hasira ziliisha na mamilioni ya watu walikimbilia katika App store na kuidownload Facebook messenger kwa lengo la kuendeleza mazungumzo yao ya facebook.Kwa hiyo hivi inakushangaza kuwa Facebook ndio App inayoongoza kushushwa kwa mwaka katika iPhone?.
Na.02. SnapChat; App ya meseji za kupotea ilianzishwa mwaka 2011. Wengi walizanii haitaweza kujipatia jina kama Apps zingine kubwa duniani. Picha Milioni 700 zinatumwa kila siku na watumiaji wa Snapchat kwa siku, Mmmh hizo ni Snap nyingi sana!
Na.03. Youtube; Site namba moja duniani kwa video. inawafikia watu bilioni 1 kwa mwezi
Na.04. Facebook; Mtandao mkubwa zaidi wa kijamii ambao una watu wengi zaidi (bilioni 1.3)
Na.05. Instagram; hapa ndipo picha milioni 60 zinakua ‘shared’ kwa siku. App hii ilizidi kuwa maarufu baada ya kuchukuliwa na facebook
Na.06. Free music with Pandora; Jumba la redio za kimtandao duniani
Na.07. Google Maps; Ramani ya dunia nzima katika kifaa chako chenye uwezo wa kuingia mtandaoni
Na.08. Flipagram; App ilianziswa mwishoni mwa mwaka 2013, inakuwezesha kugeuza picha zako za Facebook na Instagram kuwa katika video za stori.
Na.09. Spotify; Kwa miziki mingi ya mtandaoni. Bonyeza Play kwa ajili ya ‘live streaming’
Na.10. 2048; Gemu linalosisha namba (mahesabu) na hivyo linahitaji akili nyingi katika kulicheza. Pia wahariri wa Apple wamesema ndio gemu bora la mwaka.
App Zilizo Ongoza Kushushwa Katika iPad Kwa Mwaka
1. YouTube
2. Netflix
3. Calculator for iPad
4. Skype
5. Microsoft Word
6. Facebook Messenger
7. Facebook
8. Candy Crush Saga
9. Chrome browser
10. Clash of Clans
Apple kupita soko lake la App store imekua ikiwapataia watumiaji wa simu na vifaa vyake vingine kuweza kushusha Apps za bure hata zile za kuuzwa kwa kipindi kirefu sasa.
Ifuate TEKNOKONA na huku Twitter, Facebook na Instagram tafadhali
No Comment! Be the first one.