fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Infinix simu Tanzania Teknolojia Tigo

Infinix Hot 10t inapatikana Tanzania pia

Infinix Hot 10t inapatikana Tanzania pia

Spread the love

Unapoizungumzia Infinix Hot 10t ni simu janja ambayo ina wiki tu tangu kuzinduliwa kwake na tayari inaweza kupatikana nchini Tanzania kwa urahisi tuu.

Ni nadra sana kwa simu kuzinduliwa kisha kuanza kupatikana nchini Tanzania ndani ya wiki moja tangu kuzinduliwa kwake lakini hilo limewezekana kwa rununu Infinix Hot 10t ambayo kwa haraka haraka tuu ina uwezo mkubwa kwenye kamera lakini pia upande wa betri ipo vizuri.

Sifa za Infinix Hot 10t

Hii ni simu yenye uwezo ingawa si wa juu sana lakini inakidhi kwa kile ambacho soko linataka hususani kuweza kutumia simu janja vizuri kwa ajili ya kucheza gemu bila kukwamakwama. Mbali na hilo utapate kufahamu sifa zake kinagaubaga.

Kioo :
 • Ukubwa: inchi 6.82 (720 x 1640px)
 • Ubora: IPS LCD sana+umbo mithili ya tone la maji kwenye kamera ya mbele na uso wa nyuma ni plastiki
Memori :
 • Diski uhifadhi: 128GB+uwezo wa kuweka memori ya ziada
 • RAM: GB 4
Betri/Chaji :
 • Li-Ion 5000 mAh
 • Micro USB 2.0, OTG
Kipuri mama :
 • MediaTek Helio G70 SoC

Programu Endeshi

 • XOS 7.6, Android 11
Rangi
 • NyeusiKijani, Bluu, rangi ya bahari na Zambarau
  Infinix Hot 10T

  Simu hii ina teknolojia ya kutumia alama ya kidole, AI ipo pia, Bluetooth 5.0, inatumia kadi mbili za simu.

   

Kuhusu kupatikana nchini Tanzania

Infinix Hot 10T ambayo pia inakubali mtandao wa 4G Tigo Tanzania ndio wameamua kuifanya simu hii ipatikane kirahisi kwenye maduka yao nchi nzima. Pia, ina uwezo wa kudumu na chaji kwa muda wa saa 24 huku ikiwa kwenye matumizi ya intaneti. Mbali na hilo wateja watapata GB 78 za intaneti BURE kutumia kwa muda wa mwaka mmoja.

Infinix Hot 10T

Uzinduzi wa simu janja-Infinix Hot 10t nchini Tanzania.

Kuhusu bei yake ni kwamba mpaka tunaingia mtandaoni kuandaa makala hii Tigo Tanzania walikuwa bado hawajaipandisha kwenye tovuti yao lakini kwa bei ya ughaibuni inakaribia $169| zaidi ya Tsh. 390,172.

Vyanzo: Tigo Tanzania, GSMArena

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania