fbpx

Samsung yasitisha kuzalisha Galaxy J, sasa ni mwendo wa Galaxy A

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Ikiwa unatarajia simu nyingine ya Galaxy ya familia ya J kutoka kampuni ya Samsung basi hilo sahau, kwani kampuni hiyo ya Korea kusini haitatoa tena simu kwa jina la Galaxy J kwahiyo tafsiri yake ni mwendo wa Galaxy A.

Pamoja na habari hiyo kuwa mbaya kwa wapenzi wa matoleo hayo ya Galaxy J, habari njema ni kwamba watumiaji wa simu za Samsung wataendelea kupata matoleo mbalimbali ya bei nafuu zaidi. Simu za matoleo ya galaxy A na M zimezinduliwa mwaka huu kwa matoleo kadhaa.

mwendo wa Galaxy A

Kampuni ya Samsung tawi la Malaysia imetoa video mapema mwezi huu inayosema kwamba Familia ya simu za J hazitatoka tena na badala yake itakuwa mwendo wa Galaxy A.

Ingawa matoleo ya simu za Galaxy A na M yanaonekana kufanana zaidi kwa sifa zitapatikana katika masoko yote duniani kwa bei ya kiwango cha kati na chini. Samsung tayari imezindua simu tano za familia ya Galaxy A kwa mwaka huu za Galaxy A10, A20, A30, A50, na A70. Na mwezi huu wanataraji kuzindua A60, A80 na A90.

INAYOHUSIANA  Mark Zuckerberg akataa kuwa Facebook 'ilihusika' katika uchaguzi mkuu Marekani

Mbali na kusitishwa kwa matoleo ya Galaxy J, taarifa ni kwamba simu hizo zitaendelea kupata masasisho ya Android 9.0 na hata toleo lijalo la Android Q. Vipi umeipokeaje habari hii? Tupe maoni yako.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.