fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Maujanja Teknolojia Windows

Badili Picha ya Kufungua Windows 7 iwe Utakavyo na Mengineyo

Badili Picha ya Kufungua Windows 7 iwe Utakavyo na Mengineyo

Spread the love

Mtu yeyote anayeipenda kompyuta yake hupenda kuifanya ionekane tofauti na kompyuta ya mtu mwingine. Kama wewe ni mtumiaji wa Windows 7, kuna baadhi ya vitu rahisi unavyoweza kufanya kutimiza lengo hili kama kubadilisha picha ya kufungua windows 7, sauti na hata maneno kuwa kama unavyotaka wewe.

Badili muonekano unaotokea unapoanzisha WIndows

Kubadilisha picha na maneno yanayotokea unapoanzisha Windows, tumia programu ya Windows 7 Boot Updater inayopatikana kupitia tovuti ya coderforlife. Ni programu ndogo na rahisi kutumia ila ina tahadhari moja: Inawezekana usiweze kurudisha muonekano wa WIndows ilivokuwa kabla ya mabadiliko, kwahiyo, itabidi ukubaliane na hilo kabla ya kuitumia.

SOMA PIA  TikTok inajaribu kitufe cha 'repost' ili kushambaza klipu na marafiki

Badili Picha ya kufungua Windows (‘Lockscreen’)

Tumia programu iitwayo Windows 7 Logon Background Changer inayopatikana kupitia julien-manichi.com.

Background Changer ni programu ambayo ni rahisi kutumia kwa kuweka picha unayotaka na kuchagua watumiaji wa kompyuta yako wanaoweza kubadili picha hiyo.

Programu hii inafanya kazi kwenye WIndows za aina yoyote isipokuwa chache zinahitaji marekebisho kidogo ambapo programu hiyo inatoa maelekezo ya kuyakabili kirahisi.

SOMA PIA  Ndege ya huduma ya intaneti kutoka Facebook yapata ajali ktk majaribio

Badili Muito unapofungua kompyuta

Kubadili sauti inayosikika wakati Windows inaanza tumia programu ya Start up Sound Changer unayoweza kuishusha kupitia tovuti hii . Kabla ya kuweka sauti unayotaka, hakikisha unaiweka katika mfumo wa (.wav) ili ipate kuwezeshwa.

 

Picha na www.expothemes.com

ecay

Ninafuatilia teknolojia kila siku na ninapenda kutoa ujuzi wangu kuhusu teknolojia. Karibu tuzungumze kuhusu teknolojia hapa teknokona!

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania