Kampuni ya Microsoft imetangaza ujio wa simu ya bei ya rahisi zaidi kutoka kwao inayokuja na uwezo wa intaneti na kamera kwa dola 29 za kimarekani (Tsh 50,103/=).
Kwa simu hii na bei yake Microsoft wanalenga zaidi ya watu bilioni moja duniani asa kwenye bara la Afrika na Asia ambao bado hawajawahi miliki simu zenye intaneti. Lakini kwa uwezo wake na bei yake naamini watu wengi zaidi wanaopenda simu ya kawaida ila yenye uwezo wa maana watanunua simu hiyo.
Sifa Zake;
- Itakuwa na mfumo wa 2G katika intaneti.
- Itakuja na matoleo mawili moja la laini moja na jinginela la laini mbili.
- Utaweza kutumia huduma maarufu kama Facebook, Twitter, Opera Mini Browser, na Bing.
- Ina tochi
- Inauwezo wa kukaa na chaji kwa siku 29 kwa matumizi ya kawaida, siku 27 kwa toleo la laini mbili;
- Kamera (VGA) na uhifadhi wa nyimbo kwa mfumo wa mp3 (makisio ya ukubwa wa kuchukua nyimbo za hadi masaa 50 ya kucheza)
- Kioo inchi 2. (-inch QVGA LCD display) – 320 x 240 pixels
- 8 MB RAM.
Nokia 215 haijatengenezwa kwa ajili ya kukufanya uachane na simu janja za ubora zaidi, ila imetengenezwa kwa wale tunaoitaji kitu kinachofanya kazi na kudumu.
Simu hii itakuja kwa rangi 3 tofauti, zote zikiwa maarufu kwenye familia ya Nokia Lumia, nazo ni ya kijani, nyeusi na nyeupe. Tegemea kuiona simu hii sokoni ndani ya miezi hii mitatu ya mwaka 2015. Inategemewa ata baada ya kodi na gharama kadhaa kwa wafanyabiasha bei ya simu hii haitaenda mbali sana na Tsh 50,000/=
No Comment! Be the first one.